KAMPUNI ya KFC Kuku Foods Limited Tanzania wametoa msaada wa
vifaa
vya braille kwa wanafunzi wenye ulemavu wa kuona na kusikia wa shule ya
msingi Uhuru Mchanganyiko iliyopo kariakoo jijini Dar es Salaam.
Katika
halfa ya makabidhiano ya vifaa maalum kwa Shule ya Msingi Uhuru
Mchanganyiko iliopo Kariakoo, KFC Meneja Mkuu wa KFC Tanzania, Louis
Venter
amesema
kuwa vifaa hivyo vitawasaidia wanafunzi wenye mahitaji maalum ambao ni
wasio na uwezo wa kuona na wale wasioweza kusikia Vile vile Msaada huo
ni muundelezo wa ushirikiano na uhusiano wa karibu kati ya Kampuni ya
KFC na Shule ya Msingi Uhuru Mchanganyiko.
Meneja
Mkuu wa KFC Tanzania Bwana Louis Venter amesema, “ Dhumuni la Mchango
wetu ni kusaidia kuboresha mazingira ya kijamii ya watoto hawa. Tunataka
mchango huu wa kampuni yetu uwe wa maandalizi ya uzinduzi wa programu
maalum iitwayo ‘Add Hope Program’ ya kusaidia jamii nchini Tanzania
mwezi Oktoba mwaka huu.”
Kampuni ya KFC imedhamiria kutoa msaada kwa shule hii yenye mahitaji maalum kwa kipindi endelevu.
Meneja
Mkuu wa KFC Tanzania, Louis Venter akizungumza na wanafunzi wa shule ya
Msingi Uhuru Mchanganyiko pamoja na wafanyakazi pamoja na walezi wa
wanafunzi wenye ulemavu wanaosoma katika shule hiyo jijini Dar es Salaam
na kutoa msaada wa vifaa vinavyowasaidia watoto wenye ulemavu wa
macho(Upofu).
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Uhuru Mchanganyiko, Anna Mshana akizungumza mara baada ya kupokea msaada wa shule ya msingi Uhuru Mchanganyiko.
Mkuu
wa Kitengo cha Wanafunzi Walemavu katika Shule ya Msingi Uhuru
Mchanganyiko, Ahmed Abdallah akizungumza wakati wa kukabidhiwa vifaa
vya braille kwa wanafunzi wenye ulemavu wa kuona na kusikia wa shule ya
Msingi Uhuru Mchanganyiko iliyopo Kariakoo jijini Dar es Salaam.
Meneja Mkuu wa KFC Tanzania, Louis Venter akizungumza wakati wa kukabidhi wa
vifaa vya braille kwa wanafunzi wenye ulemavu wa kuona na kusikia wa
shule ya Msingi Uhuru Mchanganyiko iliyopo Kariakoo jijini Dar es
Salaam.
Baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi Uhuru Mchanganyiko wenye ulemavu
wa kuona na kusikia wakiwa katika hafla fupi ya kukabidhiwa vifaa vya braille ambavyo vitawasaidia katika masomo yao.
Baadhi ya wafanyakazi wa KFC watitoa msaada wa vifaa vya braille kwa wanafunzi wenye ulemavu wa kuona na kusikia kwa Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Uhuru Mchanganyiko, Anna Mshana jijini Dar es Salaam.
Mwalimu
Mkuu wa Shule ya Msingi Uhuru Mchanganyiko, Anna Mshana akiwa katika
picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa KFC jijini Dar es Salaam
mwishoni mwa wiki.
Mkufunzi
mmojawapo mwenye ulemavu wa kuona, Hadji Zuberi akiwashukuru waanyakazi
wa KFC kwa kuona umhimu wa kutoa masaada katika shule ya Msingi
Mchanganyiko iliyopo Kariakoo jijini Dar es Salaam leo.
No comments:
Post a Comment