Treni
ya Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) ikiwa tayari kwa kuanza safari yake
ya Jiji kuanzia Stesheni ya Dar es Salaam kwenda Pugu huduma ambayo
imeanza kutolewa rasmi jana.
TRENI
ya pili ya Jiji la Dar es salaam imeanza kutoa huduma zake kwa safari
za jiji za kuanzia Stesheni hadi pugu, ambayo itakuwa ikitoa huduma
mara 3 kwa asubuhi na mida ya jioni mara 3 ambayo itasaidia sana
kupunguza adha ya usafiri kwa wakazi wa maeneo hayo huku ikiongeza kasi
ya uchumi kwa wakazi wa maeneo ya pugu hasa wakiwemo wachuuzi.
Baadhi
ya wafanyabiashara ndogo ndogo wanaotokea maeneo ya kuanzia kipawa
mpaka Pugu, wamepngeza kuanzishwa kwa safari hiyo, kwani itawapunguzia
adha ya safari ya muda mrefu njiani na sasa watakuwa wakiwahi katika
maeneo yao ya biashara hasa wale wanaofika Soko la Kimataifa la Samaki
Ferry kuchukua Samaki, ambapo sasa watachukua usafiri wa Bajaji na
kuwahi usafiri wa treni kwa muda uliopangwa.
Wakazi wa Jiji la Dar es Salaam wakigombania kuingia katika mabehewa baada ya kuanzishwa usafiri huo.
Wanafunzi
wa Shule Mbalimbali wakiwa ndani ya mabehewa ya Treni ya Kampuni ya
Reli Tanzania (TRL) katika Stesheni ya Dar es Salaam kwenda Pugu huduma
ambayo imeanza kutolewa. (PICHA ZOTE NA KHAMISI MUSSA)
Askari
wa kike ambae jina lake halikuweza kupatikana maramoja, akidandia
behewa huku Treni ikiwa imeanza mwendo katika kituo ya Buguruni.
No comments:
Post a Comment