Mkurugenzi wa Kampuni ya Aggrey and Clifford, Rashid Tenga alielezea machache mbele ya wageni na waandishi wa habari waliohudhuria uzinduzi huo juu ya huduma mpya ya matangazo katika bara la Afrika utakaowanufaisha watangazaji, wasanii na watu maarufu uliofanyika jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Profesa Elisante Ole Gabriel na Kulia ni Mkurugenzi wa Ukuzaji Biashara wa Binary, Eni Kihedu. PICHA ZOTE NA CATHBERT KAJUNA WA KAJUNASON BLOG.
Katibu Mkuu wa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Profesa Elisante Ole Gabriel (katikati) akimsifia msanii Diamond Platinumz kwa jinsi ambavyo amekuwa akiitangaza Tanzania nje ya nchi kwa muziki wake.
Katibu Mkuu wa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Profesa Elisante Ole Gabriel akimsifia Wema Sepetu jinsi ambavyo amekuwa akilitunza jina lake.
Msanii Diamond Platinuz akitoa shukrani zake za pekee kwa niaba ya wasanii walihudhuria hafla hiyo.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Aggrey and Clifford, Rashid Tenga (kushoto) akizunguza na Katibu Mkuu wa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Profesa Elisante Ole Gabriel wakati wa uzinduzi wa huduma ya matangazo kutumia teknolojia ya kidigitali ambayo itawezesha watangazaji wa biashara kutangaza biashara zao kwa kuwatumia wasanii na watu maarufu katika jamii iliyofanyika jijini Dar es Salaam. Pembeni ni
Wageni waalikwa waliohudhuria shughuli hiyo.
Wasanii waliohudhuria shughuli hiyo.
Waandishi nao hawakuwa nyuma kufuatilia tukio.
Huduma ya matangazo kidigitali kwa kutumia wasanii na watu maarufu yaanzishwa nchini.
---
Kampuni inaoongozwa kwa kutoa huduma ya matangazo ya biashara nchini ya Aggrey & Clifford imezindua kitengo cha kutoa huduma ya matangazo kutumia teknolojia ya kidigitali ambayo itawezesha watangazaji wa biashara kutangaza biashara zao kwa kuwatumia wasanii na watu maarufu katika jamii ambayo itanufaisha pande zote zitazoshiriki kutumia huduma hii .
Huduma hii ya kisasa inayoendana na wakati wa sasa wa kizazi kipya inawezesha matangazo kuwafikia walengwa wengi na kwa haraka inasimamiwa na kampuni tanzu ya masuala ya huduma za matangazo ya biashara kwa kutumia teknolojia ya kidigitali ya Aggrey&Clifford inayojulikana kama Binary.
Uzinduzi wa kitengo hiki cha matangazo kwa kutumia teknolojia ya kisasa itakayoleta mapinduzi katika sekta ya matangazo ya biashara nchini umefanyika jana katika hoteli ya Hyatt Regency ambapo mgeni rasmi alikuwa ni Katibu Mkuu wa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Profesa Elisante Ole Gabriel na ilihudhuriwa na wataalamu wa masoko kutoka makampuni ya FMCG, huduma za mawasiliano,mabenki na taasisi mbalimbali za biashara ikiwemo wasanii na wanamichezo.
Kampuni ya Binary kwa kuanza tayari inashirikiana na wasanii na watu maarufu Zaidi zaidi ya 40 ambao miongoni mwao wapo wasanii wa filamu,wanamuziki,watangazaji maarufu wa redio na luninga. Kutokana na ushirikiano huu Binary itawatumia katika huduma za matangazo za wateja mbalimbali wanaotangaza huduma na bidhaa zao kidigitali ili kuwafikia watumiaji wa huduma/bidhaa wengi na kwa urahisi.
Huduma hii mpya ya matangazo katika bara la Afrika unanufaisha watangazaji kwa huduma zao kuwafikia wananchi ama wateja wengi kutumia umaarufu wa wasanii na watu maarufu ambao pia wananufaika kwa kupata mapato ya uhakika kutokana na kutumiwa kwao katika huduma ya matangazo na pia ina unafuu kulinganisha na njia nyingine za matangazo.
Profesa Elisante Ole Gabriel alisema kuwa serikali inao dhamira ya kuwasaidia wasanii wa tasnia mbalimbali na wanamichezo na alipongeza kuanzishwa kwa huduma hii nchini ambao itaongeza ajira na vipato vya wasanii wakati huohuo kunufaisha makampuni kwa njia ya matangazo ya biashara zao.
Naye Mkurugenzi wa Ukuzaji Biashara wa Binary, Eni Kihedu amesema “Huduma hii mpya ni jukwaa la aina yake lya matangazo ya baiashara kwa kuwa inawezesha matangazo kuwafikia walengwa kwa asilimia 100% kwa kulinganisha na kutangaza kwa kutumia magazeti na ama majarida na inaleta unafuu kwa watangazaji ambao kwa kutumia mtandao wasanii zaidi ya 40 ambao tunashirikiana nao kupitia akaunti zao za mitandao ya kijamii matangazo yataweza kuwafikia watumiaji wa bidhaa na huduma zaidi ya milioni 20 nchini na tunao uwezo wa kufikia watu wengi zaidi”.
Kuhusiana na huduma hii mpya ya matangazo itakavyonufaisha wasanii Kihedu alisema “Tunatumia fursa ya kutumia teknolojia ya digitali katika biashara ambayo itaongeza vipato vyao wakati huohuo vipaji vyao kuendelea kuonekana kwa watu wengi katika jamii na kuwawezesha kuwekeza zaidi kwenye fani yao na tasnia yao”
Aliongeza kuwa ushirikiano wa Binary na wasanii katika huduma za matangazo utafanyika kwa uwazi na kunufaisha pande zote na kutafanyika makubaliano maalumu ya malipo kutokana na viwango vinavyotozwa kwa kila tangazo litakalowekwa kwenye akaunti za mitandao yao ya kijamii na kulingana na wafuasi wanaotembelea akaunti zao.
“Viwango vya matangazo viko wazi kwa watangazaji na wasanii hivyo tunaamini kila upande utanufaika inavyostahili .Tunaamini njia hii ni jukwaa la aina yake kwa watangazaji kufikisha matangazo yao kwa wateja wanaowalenga kwa kuwa njia zilizokuwa zinatumika awali kutangaza hazina nafasi tena kutokana na mabadiliko ya tekonolojia“.Alisema
No comments:
Post a Comment