Teknolojia / Habari : Waziri, Nape Nnauye afungua rasmi studio za radio ya Jamii katika chuo Kikuu Huria, Kinondoni Jijini Dar - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633

Tuesday, 28 June 2016

Teknolojia / Habari : Waziri, Nape Nnauye afungua rasmi studio za radio ya Jamii katika chuo Kikuu Huria, Kinondoni Jijini Dar


 Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Nape Nnauye akikata utepe kuashiria ufunguzi wa Studio ya Radio ya Jamii iliyopo katika Chuo Kikuu Huria nchini (OUT), Kinondoni Jijini Dar es salaam leo Juni 27, 2016.  Kulia ni Mkuu wa ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues akifuatiwa na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Huria Tanzania (OUT), Prof. Elias Bisanda. Studio hiyo ni moja kati ya Studio nyingi za Radio za Jamii zilizopo maeneo mbali mbali hapa nchini, zinazodhaminiwa na Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) kwa kushirikiana na Mtandao wa Radio za Jamii Tanzania (COMNETA). 
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Nape Nnauye akizungumza katika kipindi cha moja kwa moja cha Redio ya Jamii iliyopo katika Chuo Kikuu Huria nchini (OUT), mara baada ya kuifungua rasmi Studio hiyo, Kinondoni Jijini Dar es salaam leo Juni 27, 2016. Kulia kwake ni Mkuu wa ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues akifuatiwa na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Huria Tanzania (OUT), Prof. Elias Bisanda.
Mkuu wa ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues, akitoa hotuba yake wakati wa hafla ya ufunfunguzi wa Studio Studio ya Radio ya Jamii iliyopo katika Chuo Kikuu Huria nchini (OUT), Kinondoni Jijini Dar es salaam leo Juni 27, 2016.
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Huria Tanzania (OUT), Prof. Elias Bisanda akizungumza wakati wa hafla ya ufunfunguzi wa Studio Studio ya Radio ya Jamii iliyopo katika Chuo Kikuu Huria nchini (OUT), Kinondoni Jijini Dar es salaam leo Juni 27, 2016.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Nape Nnauye akitoa hotuba yake wakati wa hafla ya ufunfunguzi wa Studio Studio ya Radio ya Jamii iliyopo katika Chuo Kikuu Huria nchini (OUT), Kinondoni Jijini Dar es salaam leo Juni 27, 2016.
Mwenyekiti wa Mtandao wa Radio za Jamii Tanzania (COMNETA), Joseph Sekiku akitoa maelezo mafupi juu ya Radio za Jamii na umuhimu wake kwa taifa, wakati wa hafla ya ufunfunguzi wa Studio Studio ya Radio ya Jamii iliyopo katika Chuo Kikuu Huria nchini (OUT), Kinondoni Jijini Dar es salaam leo Juni 27, 2016.
Mkurugenzi wa Masoko na Mawasiliano wa Chuo Kikuu Huria nchini, Mohamed Mkonongo akiongoza hafla hiyo, iliyofanyika Chuoni hapo, leo Juni 27, 2016.

No comments:

Post a Comment