Mwezi Mtukufu : Mashindano ya Kuhifadhi Qur-an Zanzibar Masjid Loota Kiembesamaki Zanzibar. - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633

Wednesday, 15 June 2016

Mwezi Mtukufu : Mashindano ya Kuhifadhi Qur-an Zanzibar Masjid Loota Kiembesamaki Zanzibar.


 
Mgeni rasmin katika Uzinduzi wa Mashindano ya Kitaifa ya Kuhifadhi Qura-an Zanzibar yalioandaliwa na Jumuiya ya Kihifadhi Quran Zanzibar Naibu Kadhi Mkuu Zanzibar Shekh.Hassan Othma Ngwali(katikati) Amiri wa Jumuiya ya  Kuhifadhi Quran Zanzibar Mwalim Suleiman Omar Naimi Amiri Kuhifadhisha Quran Zanzibar Shekh. Mohammed Alawi Ally, wakifuatilia mashindano hayo yaliowashirikisha Wanafunzi wa Vyuo vya Quran Zanzibar,Tanga Pwani na Morogoro. 
Viongozi wa Jumuiya ya Kuhifadhisha Qur-an Zanzibar wakifuatilia mashindano hayo yanayofanyika katika Masjid Loota Kiembesamaki Zanzibar na kuwashirikisha Vijana wa Umri mbali. 
Viongozi wa Kamati ya Kuhifadhi Qur-an  wakiwa katikac Masjid Loota Kiembesamaki wakifuatilia Wanafunzi wakisoma Qur-an wakati wa mashindano hayo yalioandaliwa na Jumuiya ya Kuhifadhisha Qur-an Zanzibar.
Washiriki wa Mashindano ya Kuhifadhi Qur-an Zanzibar wakiwa katika Masjid Loota wakisubiri zamu zao kushiriki mashindano hayo. yanayoshindanisha Wahifadhi Qur-an Juzuu 5.10,20 na 25.
Waumini wa Dini ya Kiislam Zanzibar wakifuatilia mashindano ya kuhifadhi Qur-an yanayofanyika katika Masjid Loota Kiembesamaki Unguja Wilaya ya Magharibi B Unguja.
Majaji wa Mashindano ya Kuhifadhi Qur-an Zanzibar wakiwa makini kufuatilia usomani wa Wanafunzi hao katika mashindano hayo. 
Watoa Aya za Qur-an kwa Washiriki wa Mashindano ya Kuhifadhi Qur-an Zanzibar wakitoa Aya kwa Washiriki hao.
Mshinriki wa Mashindano ya Kuhifadhi Qur-an Juzuu 10 kutoka Zanzibar Mwanafunzi Khayyam Mohammed mwenye umri wa miaka 13. akisoma Qur-an wakati wa mashindano hayo yanayofanyika katika Masjid Loota Kiembesamaki leo 14/6/2016.
Mwanafunzi kutoka Zanzibar Mussa Hamad mwenye umri wa miaka 9 akishiriki katika mashindano hayo ya kuhifadhi Juzuu 10, yanayofanyika katika Masjid Loota kiembesamaki Unguja 
Mshiriki wa Mashindano ya Kuhifadhi Qur-an kutoka Zanzibar Mwanafunzi Shakir Hamad Juma. akisoma Qur-an katika mashindano hayo yalioandaliwa na Jumuiya ya Kuhifadhi Qur-an Zanzibar. yaliowashirikisha Wanafunzi 27 Kutoka Zanzibar, Tanga, Pwani na Morogoro.

Imetayarishwa na Mtandao wa Zanzinews.com.
Email othmanmaulid@gmail.com - Zanzibar.

No comments:

Post a Comment