Madiwani 24 wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru wakiwa katika Mahakama ya
Hakimu Mkazi Arusha wakisubiri kusomewa shitaka la kuharibu uzio wa
eneo la Indumi Makere uzio wenye thamani ya shilingi milioni 7 .Kufuatia
mgogoro juu ya umiliki wa shamba hilo lililokua likimilikiwa na
halmashauri,Kesi ya madiwani hao itatajwa tena Juni 28 mwaka huu.Picha
na Ferdinand Shayo
Na Ferdinand Shayo wa Wazalendo 25 Blog,Arusha.
Madiwani 24
wa Halmashauri ya Wilaya Ya Meru wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi
iliyoko jijini Arusha na kusomewa mashtaka ya kuharibu uzio wenye thamani ya
shilingi milioni 7 kwenye eneo linalomilikiwa na Itandumi Makere.
Madiwani hao
waliofikishwa mbele ya Hakimu Mkazi Agustine Rwizeli wamekana mashtaka hayo na
kudai kutohusika na kitendo hicho.
Wakili wa
Anayewawakilisha madiwani hao Charles Abraham amesema kuwa kesi hiyo itatajwa
tena juni 28 mwaka huu katika Mahakama hiyo.
Wakati huo
huo Mahakama hiyo imetoa hukumu kwa aliyekua akituhumiwa kumkashifu Rais John
Pombe Magufuli kwa kutumia mtandao wa Facebook ,Izack Habakuki mwenye umri wa miaka 40,ambapo
baada ya kupatikana na hatia hukumu imetolewa na ameamuriwa kulipa kiasi cha
shilingi milioni 7 kama adhabu na iwapo atashindwa kulipa atatumikia kifungo
cha miaka 3 jela kwa mujibu wa sheria ya mtandao ya mwaka 2015 kifungu cha 6.
Wakili wa
TCRA Johaness Karungura amewataka Watanzania kujihadhari na matumizi mabaya ya
mitandao ambayo yanaweza kuwaingiza katika matatizo hivyo kuitumia mitandao
hiyo kwa manufaa.
No comments:
Post a Comment