Matukio : Mhe. Samia Suluhu azindua kituo cha kisasa cha huduma ya magari, Jijini Arusha - Wazalendo 25 Blog

Habari Mpya

Glory to Story.


Post Top Ad


14 May 2016

Matukio : Mhe. Samia Suluhu azindua kituo cha kisasa cha huduma ya magari, Jijini Arusha


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe, Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro Mhe. Said Meck Saddik alipowasili Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro kwa ajili ya kuanza ziara ya kikazi ya siku tatuMkoani Arusha, baada ya kukamilisha zira yake ya kikazi katika Mikoa ya Mwanza na Geita. Katikati Mkuu wa Mkoa Arusha Mhe. Daud Felix Ntibenda.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Viongozi na Makamanda wa Kamati za Ulinzi na Usalama za Mikoa ya Kilimanjaro na Arusha alipowasili Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro kwa ajili ya kuanza ziara ya kikazi ya siku tatu Mkoani Arusha, baada ya kukamilisha zira yake ya kikazi katika Mikoa ya Mwanza na Geita.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiangalia Vikundi vya Ngoma za aina mbalimbali
alipowasili Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro kwa ajili ya kuanza ziara ya kikazi ya siku tatu Mkoani Arusha, baada ya kukamilisha zira yake ya kikazi katika Mikoa ya Mwanza na Geita.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiangalia Matairi ya Magari aina ya BF Goodrich KO2 yanayosambazwa na kampuni ya Superdoll baada kuwasili katika kituo cha kisasa cha huduma za magari na Matairi cha Superdoll mjini
Arusha kwa ajili ya kuzindua rasmi kituo hicho. Kusshoto Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Superdoll Seif Ali Seif. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akibonyeza kitufe na kupata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Superdoll Seif Ali Seif alipokua akizindua rasmi kituo cha kisasa cha huduma za magari pamoja na Matairi cha Superdoll mjini Arusha.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Superdoll Seif Ali Seif baada ya kuzindua rasmi kituo cha kisasa cha huduma za magari pamoja na Matairi cha Superdoll mjini Arusha.
(Picha na OMR)

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad