Matukio : Mamia wajitokeza kumuaga Mwanahabari Makongoro Oging' kuzikwa Mkoani Mara kesho kutwa - Wazalendo 25 Blog

Breaking

Glory to Story.


Post Top Ad


26 May 2016

Matukio : Mamia wajitokeza kumuaga Mwanahabari Makongoro Oging' kuzikwa Mkoani Mara kesho kutwa

 Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Global Publishers alikokuwa akifanyia kazi Makongoro Oging', Eric Shigongo akitoa heshima za mwisho mbele ya jeneza lenye lenye mwili wa marehemu Oging' wakati wa kuagwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Ilala ya Amana Dar es Salaam mchana wa leo.
 Mmiliki wa Blog ya Michuzi, Issa Michuzi akitoa heshima za kwa mwili wa marehemu.
 Mhariri wa Habari wa Gazeti la Champion, Salehe Ali akitoa heshima za mwisho kwa marehemu.
 Waombolezaji wakiwa na huzuni wakati wa kuaga mwili wa mpendwa wao Makongoro.
 Mtangazaji wa Kituo cha Televisheni cha ITV. Sam Mahela akitoa heshima za mwisho.
 Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri wa Habari Tanzania (TEF), Absalom Kibanda akiwa kwenye shughuli hiyo ya kumuaga Makongoro Oging'
 Ndugu yake na Makongoro Oging' akilia wakati wa kumuaga mpendwa wake Makongoro.
 Ndugu jamaa na marafiki wakiwa kwenye uagaji wa mpendwa wao.
 Uagaji ukiendelea.
 Mtoto wa marehemu akimuaga baba yake 'hakika ni huzuni kubwa'
 Mjane wa marehemu akiwa hajiwezi baada ya kumuaga mume wake.
 Mhariri wa habari wa gazeti la Uwazi alilokuwa akiandikia marehemu Oging' Elvan Stambuli akilia kwa uchungu wakati wa kumuaga Makongoro.
 Baba mlezi wa Makongoro Oging ambaye alimsomesha, akizungumza na wanahabari.
Waombolezaji wakiwa wamebeba jeneza lenye mwili wa Makongoro kulipeleka kwenye gari kabla ya kuanza kwa safari ya kwenda mkoani Mara.
Jeneza likiingizwa kwenye gari tayari kwa safari.

Post Top Ad