NA VERO IGNATUS wa Wazalendo 25 Blog, ARUSHA.
Mtu mmoja anayefahamika kwa jina la Ibrahimu Juma Selemani Kathembe (33) ,amefikishwa katika mahakama ya wilaya ya Arusha kwa tuhuma za kufanya utapeli wa kukusanya ushuru wa mabango jijini arusha .
Mwendesha mashtaka Sabina Silayo akisoma shtaka hilo mbele ya Hakimu Mkazi Mh Ally Athumani Jasmine katika mahakama hiyo ,amesema kuwa Ibrahimu Juma Selemani Kathembe anakabiliwa na makosa 3
Akitaja makosa hayo amesema kosa la (1) ni kugushi risiti ya malipo ya ushuru wa mabango , kosa la (2) kufoji kuwa ni wakala wa kukusanya mapato wa Halmashauri ya jiji , na kosa la (3 ) likiwa ni kujipatia pesa kwa njia ya udanganyifu
Mshitakiwa anadaiwa kutenda makosa hayo tarehe 8 na 9 februaAri Jijini arusha ,ikiwa ni pamoja na kujipatia pesa kwa njia ya udanganyifu yenye thamani ya shilingi 40,000 kutoka kwa Baluvi Chanye kwa madai ni mpokea ushuru wa jiji la arusha
Mtuhumiwa alikana mashtaka hayo mbele ya hakimu Mkazi , na mahakama kuruhusu kupewa dhamana ya masharti ,ikiwa ni kudhaminiwa na watu wawili ,ambao ni watumishi wa Taasisi ya serikali pamoja na kuwasilisha hati yenye thamani ya 10 millioni kila moja.
Hata hivyo ,mshtakiwa alishindwa kutimiza masharti ya dhamana na kurudishwa rumande ambako mahakama imeamuru shauri hilo kusikilizwa tena tarehe 26 mwezi huu
Akizungumza mwanasheria anayesimamia kesi hiyo upande wa madai ambao ni Halmshauri ya Jiji la Arusha , David Makattha amesema mtuhumiwa huyo amekuwa akipita kwa wafanyabishara na kuwalipisha ushuru wa mabango yao kwa bei ya maelewano
" Mtu kama anadaiwa laki 5 yeye amekuwa akipatana nao alipwe laki 2 ,pia imekuwa ni tabia yake ,kupitia msako tulioanza mwezi oktoba 2015 tuligundua kuwa watu wengi sana wametapeliwa kwa mtindo huo anayesimamia kesi hiyo alisema mtuhumiwa huyo thamani
Nae msemaji wa jiji ,Ntengejwa Hosea amewataka wananchi wote kufwata mfumo mpya wa ulipaji wa ushuru kwanjia za kibenki na kwamba wasikubali kulipishwa na watu wanaofwata nao.
No comments:
Post a Comment