Mkurugenzi
wa Uuguzi na Ukunga wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Agness
Mtawa akisoma kiapo kwa wauguzi katika maadhimisho ya Siku ya Wauguzi
Duniani. Maadhimisho hayo yamefanyika leo katika hospitali hiyo.
Wauguzi wa hospitali hiyo wakila kiapo katika maazimisho ya Siku ya Wauguzi Duniani.
Mkurugenzi
wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Profesa Laurence Museru
akifuatilia maazimisho ya Siku ya Waaguzi Duniani yaliofanyika leo
ukumbi wa CPL kwenye hospitali hiyo.
Mwenyekiti
wa Chama Cha Wauguzi Tawi la Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH),
Sabastian Luziga akisoma risala ya wauguzi mbele ya Kaimu Mkurugenzi wa
hospitali hiyo, Profesa Laurence Museru.
Wauguzi, Cleopatra Mtei (kushoto) na Nasra Said (kulia) wa hospitali hiyo wakifuatilia risala iliyosomwa leo na mwenyekiti huyo.
Baadhi ya wauguzi wa hospitali hiyo wakifuatilia risala iliyosomwa na Mwenyekiti wa Chama Cha Wauguzi Tawi la Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Sabastian Luziga.
Baadhi ya wauguzi wa hospitali hiyo wakifuatilia risala iliyosomwa na Mwenyekiti wa Chama Cha Wauguzi Tawi la Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Sabastian Luziga.
PICHA NA JOHN STEPHEN, HOSPITALI YA TAIFA YA MUHIMBILI (MNH)
KAIMU
Mkurugenzi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Profesa Lawrence
Museru amewakumbusha wauguzi kufanya kazi kwa kufuata maadili na misingi
ya taaluma yao na kuwafichua wachache ambao wanaenda kinyume na maadili
kazi ili hatua stahiki zichukuliwe.
Profesa
Museru ametoa wito huo leo katika maadhimisho ya Siku ya Wauguzi
Duaniani , ambapo wauguzi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili leo
wameadhimisha siku hiyo.
Katika
maadhimisho hayo Profesa Museru amewasisitiza wauguzi hao kutambua
kwamba muuguzi ni mtu muhimu katika kutoa huduma, hivyo hawana budi
kuwahudumia wagonjwa kwa moyo ili kuondoa malalamiko.
“
Nawaomba muwafichue wale wachache ambao wanatoa lugha zisizofaa kwa
wagonjwa kwani mkifanya hivyo mtatusaidia sana kuondoa kero na
malalamiko yanayotolewa dhidi yenu,” amesema Profesa Museru.
Mipango ya Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Akielezea
mipango ya MNH Profesa Museru amesema Hospitali hiyo ina mpango wa
kuwaendeleza kitaaluma watumishi wake wakiwemo wauguzi ili watoe huduma
yenye kiwango cha juu zaidi.
Mpango
mwingine ni kuboresha sehemu za kufanyia kazi, kununua vifaa tiba
kadiri fedha zinavyopatikana pamoja na kutafuta kibali kwa lengo la
kuajiri wauguzi wengine ili wasaidie kutoa huduma kwani wauguzi waliopo
sasa hawatoshelezi mahitaji.
Kutekeleza agizo la Rais
Kwa
mujibu wa Profesa Museru Hospitali ya Taifa Muhimbili imefanya
mabadiliko makubwa katika kutekeleza agizo la Rais Dk John Magufuli na
kuhakikisha kwamba wagonjwa wanaokuja kutibiwa MNH wanapata dawa na
kupata vipimo kwa wakati.
Hivyo ametoa wito kwa wauguzi kushiriki katika jitihada zote zinazofanywa na Hospitali katika kuongeza mapato ya hospitali hiyo.
Akisoma
risala ya wauguzi, Mwenyekeiti wa chama cha wauguzi Tawi la MNH,
Sebastian Luziga amesema changamoto inayowakabili ni kuwapo kwa idadi
ndogo ya wauguzi hali inayoathiri utendaji kazi.
“Idadi
ya wauguzi ni ndogo ukilinganisha na idadi ya wagonjwa kwani kwa siku
muuguzi anahudumia wagonjwa kati ya 20 hadi 30 tofauti na uwiano ambao
muuguzi mmoja anatakiwa kuhudumia wagonjwa 6 hadi 8 kwa siku.” Amesema
Sebastian.
Kauli mbiu ya siku ya wauguzi Duniani mwaka huu ni “Wauguzi Nguvu ya Mabadiliko, Uboreshaji wa uthabiti wa mifumo ya afya”
Mei 12 wauguzi wote Duniani wanamkumbuka muasisi wa uuguzi mama Florence Ningtngale.
No comments:
Post a Comment