Utalii Wetu : TANAPA kuzindua kampeni ya kufanya usafi Mlima Kilimanjaro - Wazalendo 25 Blog

Habari Mpya

Glory to Story.


Post Top Ad


20 Apr 2016

Utalii Wetu : TANAPA kuzindua kampeni ya kufanya usafi Mlima Kilimanjaro


Meneja Mawasiliano wa Tanapa ,Pascal Shelutete akizungumza na Waandishi wa Habari (hawapo pichani) juu ya kampeni ya kufanya usafi katika Hifadhi ya Mlima Kilimajaro akizungumza na Waandishi wa Habari jana katika Makao Makuu ya Tanapa,kushoto ni Katibu Mkuu wa Chama cha Mawakala wa Utalii Sirili Akko,kushoto ni Afisa Masoko wa Hoteli ya Kibo Palace Jenipher.Picha na Ferdinand Shayo



Shirika la Hifadhi za Taifa TANAPA limejipanga kuzindua kampeni ya kitaifa ya  kufanya usafi mlima Kilimanjaro ambao unakusanya mapato ya shilingi bilioni 60 kwa mwaka na kuajiri Watanzania laki 3.

Meneja Mawasiliano wa TANAPA Pascal Shelutete akizungumza na Waandishi wa Habari amesema kuwa kampeni hiyo itasaidia kuboresha mazingira safi ya Hifadhi ya Mlima Kilimanjaro na kuinusuru na uchafuzi wa mazingira wa kidunia (Global warming), Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA), inatarajia kuzindua kampeni ya usafi wa mlima Kilimanjaro kesho ambayo itadumu kwa siku kumi.

“Tumeamua kufanya usafi katika mlima huo ikiwa ni jitihada za kuunga mkono juhudi za Rais John Pombe Magufuli katika kuweka mazingira katika hali ya usafi hususan hifadhi za taifa” Alisema Shelutete



Katibu Mkuu wa Chama cha Mawakala wa Utalii Sirili Akko amesema kuwa mashirika binafsi yaliyoko kwenye sekta ya utalii hayana budi kushiriki katika kufanya usafi katika mlima huo wa kwanza kwa urefu barani Afrika na wapili duniani.

Pia ameitaka serikali kusimamia maagizo ya Ofisi Makamu wa Raisi Mazingira kwa kupiga marufuku ya matumizi plastiki katika hifadhi za taifa ili kuepuka kuchafua mazingira.

Mdau wa Masuala ya Utalii ambaye ni Afisa Masoko wa Hoteli ya Kibo Palace Jenipher Swai amesema kuwa wameungana na Tanapa kufanya usafi kwa kutoa vifaa vya kufanyia usafi pamoja na kushiriki kupanda mlima huo katika madhimisho ya miaka kumi ya kuanzishwa kwa hoteli hiyo.

Jumla ya Watalii 50000 hutembelea Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro na kuchangia shilingi bilioni 60,kampeni ya kufanya usafi ya muda wa siku 10 itanza kesho ikiwashirikisha wapagazi,waongoza watalii na wadau wa utalii ,kuhakikisha hali ya usafi katika hifadhi zetu zitasaidia kuvutia watalii zaidi.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad