Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi mkoa wa
Arusha Lekule Laizer akiwa anaongea na wananchi wa tawi la chama cha
mapinduzi Simba lililopo ndani ya kata ya
Mbulumbulu
Katibu
wa itikadi na uenezi wa mkoa wa Arusha Shabani Mdoe akiwa anaongea na
wananchi wa kata ya mbulumbulu wakati wa ziara ya viongozi wa mkoa wa
chama cha mapinduzi
Katibu wa itikadi na uenezi wa mkoa wa
Arusha Shabani Mdoe akiwa anaongea na wananchi wa kata ya mbulumbulu
wakati wa ziara ya viongozi wa mkoa wa chama cha
mapinduzi
Katibu wa ccm wialaya ya karatu Loth
Olelemeiruti akiwa anaongea na
wananchi
mmoja wa wananchi wa kata ya
mbulumbulu akiwa anamueleza mwenyekiti wa chama cha mapinduzi mkoa wa
Arusha matatizo yanayowakabili katika kata yao ikiwemo
ukosefu wa barabara
Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi mkoa wa
Arusha Lekule Laizer akiwa na baadhi ya viongozi wa matawi wa ccm wa
kata ya mbulumbulu wilayani karatu mkoani
Arusha
Na
Woinde
Shizza,Karatu
Mwenyekiti wa
chama cha mapinduzi mkoa wa Arusha Lekule Laizer
amewaagiza viongozi wa matawi wa
kata ya mbulumbulu na wilaya ya karatu kwa
ujumla kufanya tadhimini ya uchaguzi
uliopita haraka iwezekanavyo na kupeleka majibu kwa
katibu wa chama cha hicho wilaya ya
karatu Loth Olelemeiruti ili
kuweza kujua ni watu gani ambao waliweza
kuhujumu chama na kuchukuliwa hatua kali.
Hayo aliyasema
jana wakati alipokuwa akiongea na
wanachama wa chama cha mapinduzi ndani
ya kijiji cha Losteti kilichopo
ndani ya kata ya mbulumbulu
wilayani Karatu Mkoani Arusha .
Alisema kuwa
katika uchaguziwa uliopita baadhi ya viongozi
pamoja na wananchama waliweza kusaliti chama kwa kutoa siri za chama pamoja na
kuwapa ushirikiano viongozi wa upinzani hali ambayo ilichangia kwa kiasi
kikubwa kupoteza baadhi ya kata.
“napenda
kuwaambia viongozi wote wa matawi wafanye tadhimini
haraka iwezekanavyo baada ya hapo wapeleke majibu kwa katibu wa wilaya ya
karatu ili aweze kuyafikisha mkoani na sisi tuweze kuyatumbua majipu yote
ambayo walikisaliti chama wakati wa
kampeni”alisema Laizer
Aidha aliongeza
kuwa sasa ivi viongozi wa chama wanatakiwa
kufanya kazi kama kwa nguvu zao zote pamoja na akili zao zote ili kuhakikisha
chama kinarudi katika mstaari wake na sio hivyo tu iwapo viongozi watafanya
kazi kwa nguvu zao zote itasaidia pia kumpa nguvu rais wa nchi ambaye ametoka
katika chama cha mapinduzi.
“tunajua watu
wengi walichukuliwa na mafuriko sasa napenda
kusema yale mafuriko yameisha sasaivi ni kazi tu ,na pia napenda kutumia fursa
hii kuwaambia wananchi yeyote ambaye anataka kuwa mwana chama wa ccm achukuwe
kadi mapema kwani itafikia mahali chama akitatoa kadi tena na sio kuchukuwa
kadi tu bali kulipia ada maaana mwanachama ambaye ajalipa ada ya uanachama basi
yeye sio mwananchama hai kwakua ajalipa ada ni bei ndogo sana kwa iyo kila
mwanachama anatakiwa alipe ada ili awe mwanachama hai”alisema
Laizer
Alibainisha
kuwa kwa sasa amana kiongozi ambaye atachaguliwa
kwa kutegemea rushwa hivyo ,kama kunamwananchi au mwanachama ambaye anategemea
aje achukuwe fomu katika chaguzi zijazo kwa kutoa rushwa au anategemea atatumia
pesa zake kushinda katika uchaguzi asahau kabisa maana sasa ivi ndani ya ccm
awataki watu ambao wanatumia fedha kupat a nafasi za
uongozi wamepotea kwani aita kubalika
kabisa.
Hata hivyo mwenyekiti
huyo amejinasibu kuwa aliyekuwa mgombea wa urais kupitia umoja wa vyama
vinavyounda ukawa Edwad lowasa kamwe
atakaa aje kuwa rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania kulingana na mazambi
yake aliyoyafanya kwani amefanya
nae kazi kwa muda mrefu na
anafahamu vizuri.
Kw aupande wake
katibu wa itikadi na uenezi mkoa wa Arusha
Shabani Mdoe amesema kuwa wao kama viongozi wa chama wamejitoa sadaka kwa ajili
ya kuimarisha chama cha mapinduzi mkoa
wa Arusha na watafanya kila jitiada kuhakikisha chama kina simama imara na
iwapo kunamtu ndani ya chama anaejijua kuwa ni jipu aanze kujitumbua mapema
kabla ajatumbuliwa .
No comments:
Post a Comment