Kikosi cha
timu ya Taifa ya Tanzania kinanchoshiriki katika mashindano ya Cana
Kanda ya nne. kutoka kulia ni Amani Doggart, Catherine Mason, Hilal
Hilal na Smriti Gokarn.
Na Mwandishi wetu
Muogeleaji
wa Tanzania, Hilal Hilal ametwaa medali ya Shaba katika mashindano ya
kuogea ya Cana Kanda ya Nne yanayoendelea nchini Mauritius.
Hilal
ambaye ni nahodha wa timu ya Taifa katika mchezo huo, amemaliza katika
nafasi ya tatu katika staili ya butterfly kwa kutumia muda wa sekunde
26.70 katika mashindano hayo magumu yaliyoshirikisha nchi za Uganda,
Kenya, Rwanda Burundi, Djibouti, Eritrea, Ethiopia, Somalia, Sudani
Kusini na Sudan.
Nafasi
ya kwanza ilichukuliwa na muogeleaji kutoka Zambia, Ralph Goveia
aliyetumia muda wa 25.11 na kupata medali ya dhahabu huku Tom Donker
wa Zambia pia akimaliza katika nafasi ya pili kwa kutumia muda wa 25.66
na kupata medali ya fedha.
Hilal
pia alishiriki katika mashindano ya mita 50 ya staili ya backstroke na
kumaliza katika nafasi ya saba kati ya waogeleaji 13 kwa waogeleaji
wenye umri zaidi ya miaka 17. Hilal alitumia muda wa 29.91 katika
mashindano hayo ambapo Mzambia Tom Donker alishinda medali ya dhahabu
kwa kutumia muda wa sekunde 27.40.
Mbali
ya Hilal, muogeleaji mwingine wa Tanzania Catherine Mason alimaliza
katika nafasi ya nne katika mashindano ya mita 50 butterfly kwa kutumia
muda wa 31.89 kwa wasichana wenye umri wa zaidi ya miaka 17. Catherine
pia alimaliza katika nafasi ya nne katika mashindano ya mita 50 ya
staili ya backstroke kwa kutumia muda wa 34.13.
Pia
muogeleaji wa klabu maarufu ya Dar Swim Club (DSC) , Smriti Gokarn
alishika nafasi ya 14 kati ya waogeaji 18 katika mashindano ya mita 200
ya backstroke kwa kutumia muda wa 3.21.30.
Muogeleaji
huyo pia alishika nafasi ya tisa kwa kumia muda wa 2.31.31 katika
mashindano ya freestyle mita 200 na katika mita 50 butterfly alimaliza
katika nafasi ya 11 kwa kutumia muda wa 34.28. Pia alimaliza katika
nafasi ya 11 katika mita 50 kwa upande wa staili ya backstroke kwa
kutumia muda wa 36.43.
Naye
Amani Doggart alianza kwa kushika nafasi ya 14 katika staili ya
butterfly kwa kutumia muda wa 38.54 na baadaye kumaliza wa Saba katika
staili ya backstroke kwa kutumia muda wa 37.41 katika mashindano ya
mita 50.
No comments:
Post a Comment