Mkurugenzi
wa Uuguzi na Ukunga, Agnes Mtawa katika Hospitali ya Taifa ya
Muhimbili (MNH) akizungumza na wafanyakazi wa DAWASCO na Muhimbili kabla
ya kuanza kwa shughuli ya usafi kwenye hospitali hiyo.
Kushoto ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa DAWASCO, Mhandisi Cyprian Luhemeja.
Wafanyakazi wa DAWASCO na Muhimbili wakimsikiliza Mkurugenzi wa Uuguzi na Ukunga, Agnes Mtawa wa hospitali hiyo.
Wafanyakazi wa DAWASCO wakiendelea na shughuli za usafi katika Hospiyali hiyo.
Wafanyakazi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) na DAWASCO wakifanya usafi katika hospitali hiyo.
Gari la kutoa maji taka nalo halikuwa nyuma kwani DAWASCO na Muhimbili wamehakikisha usafi wa uhakika unafanyika.
Wafanyakazi wa DAWASCO wakikusanya takataka wakati shughuli za usafi zikiendelea katika hospitali hiyo.
Mkuu
wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi akikabidhi msaada kwa Mkurugenzi wa
Uuguzi na Ukunga, Agnes Mtawa katika Hospitali hiyo baada ya kumalizika
kwa shughuli za usafi leo asubuhi. Kulia ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa
DAWASCO, Mhandisi Cyprian Luhemeja.
Picha zote na John Stephen, Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH)
SHIRIKA
la Majisafi na Majitaka Dar es salaam (DAWASCO) limefanya usafi
katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kwa lengo la kudumisha
ushirikiano, lakini pia kutekeleza agizo la Rais Dk John Magufuli la
kufanya usafi katika maeneo mbalimbali nchini.
Usafi
huo umeongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi , Mkurugenzi
wa Uuguzi na Ukunga wa Muhimbili, Agnes Mtawa pamoja na Afisa Mtendaji
Mkuu wa DAWASCO Mhandisi Cyprian Luhemeja.
Usafi huo umefanyika katika maeneo yote muhimu ya Hospitali ikiwemo utoaji wa maji taka .
Akizungumza
mara baada ya zoezi hilo, Mkuu wa wilaya ya Ilala Raymond Mushi
amesema zoezi la kufanya usafi lazima halina budi kuwa endelevu ili
kuhakikisha maeneo yote yanakua safi lakini pia epuka magonjwa ya
mlipuko ikiwemo kipindupindu.
Kwa
upande wake Mkurugenzi Mtawa amewashukuru DAWASCO kwa uamuzi wa kuja
kufanya usafi MNH ambapo ametumia fursa hiyo pia kuwaomba wafanyakazi
wa Shirika hilo kujitolea kuchangia damu ili kuokoa maisha ya wagonjwa
ambao wanahitaji damu.
Pamoja
na mambo mengine DAWASCO wametoa msaada wa vitu mbalimbali kwa ajili ya
wagonjwa ambao wamelazwa Hospitalini hapo ambao wanapatiwa matibabu .
Neema Mwangomo, Afisa Uhusiano, MNH.
No comments:
Post a Comment