Matukio : Mchezaji wa zamani wa Nigeria Kanu atoa Msaada kwa watoto wenye mahitaji maalumu, Jijini Dar - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633

Saturday, 9 April 2016

demo-image

Matukio : Mchezaji wa zamani wa Nigeria Kanu atoa Msaada kwa watoto wenye mahitaji maalumu, Jijini Dar



1
Mchezaji wa zamani wa timu ya Taifa ya Nigeria, Super Eagles, Nwankwo Kanu (wa pili kushoto), akitoka kusaini  kitabu cha wageni katika Shule ya Msingi ya Majimatitu baada ya kufika shuleni hapo leo asubuhi kutoa msaada kwa watoto wenye mahitaji maalumu wanao soma kwenye shule hiyo. Kushoto kwake ni Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo, Abdul Mgomi. Wengine ni walinzi wake.
Picha na habari na Dotto Mwaibale

2
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Maji Matitu Bw.  Abdul Mgomi akimkaribisha mchezaji huyo shuleni hapo. Kutoka kulia ni Mwalimu Shabani Msabaha wa shule hiyo, Mchezaji Kanu na Makamu Rais wa Kampuni ya StarTimes, Zuhura Hanif.

3
Mchezaji Kanu akizungumza katika hafla hiyo kabla ya kukabidhi msaada huo.
4
Hapa Kanu akimkabidhi msaada wa sabuni ya unga Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo, Abdul Mgomi.
IMG_0460
Wanafunzi wenye mahitaji maalumu wa shule hiyo wakiwa kwenye hafla hiyo.
IMG_0469
Wazazi wa watoto wa shule hiyo wakiwa kwenye hafla hiyo.
IMG_0480
Kanu akitoa msaada wa magodoro.
IMG_0489
Kanu akitoa msaada wa vyombo vya jikoni kwa wanafunzi hao.
IMG_0492
Hapa Kanu akikabidhi unga wanafunzi hao. Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha watoto hao, Rehema Lemway na kulia kwake ni Mlezi wa watoto hao, Somoe Said Omary.
IMG_0497
Kanu akiwakabidhi wanafunzi hao Luninga.
IMG_0504
Kanu akiwa katika picha ya pamoja na watoto hao.
IMG_0514
Kanu akishiriki kucheza na watoto hao wakati wakitoa burudani.
IMG_0522
Kanu akiwa katika picha ya pamoja na wazazi wa watoto hao.
IMG_0526
Hapa Kanu akiwa katika picha ya pamoja na walimu wa shule hiyo.

No comments:

Post a Comment

Contact Form

Name

Email *

Message *

Tuwasiliane

Name

Email *

Message *