Matukio : Blogger Kajunason Asheherekea siku yake ya kuzaliwa na watoto yatima wa kituo cha SOS - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633

Monday, 11 April 2016

demo-image

Matukio : Blogger Kajunason Asheherekea siku yake ya kuzaliwa na watoto yatima wa kituo cha SOS


DSC_0167
 Mmiliki wa Kajunason Blog, Cathbert Angelo Kajuna (mwenye shati nyeupe) akimkabidhi mwakilishi wa kituo cha SOS Children's Village Tanzania Bi. Sherry Mavura (wa kwanza kulia) msaada wa vitu mbali mbali ikiwemo Sabuni, Unga, Mchele, Mafuta, miswaki, dawa za meno kwa ajili ya kuwasaidia kuendesha kituo hicho.
"Leo mchana Aprili 10, 2016 nimesherekea siku yangu ya kuzaliwa na kutimiza miaka 10 ya Uandishi wa Habari na watoto Yatima wa kituo cha SOS Children's Village Tanzania kilichopo Karibu na kituo cha mabasi cha mawasiliano (SIMU 2000) jijini Dar kwa kula nao chakula, kucheza nao ikiwa ni pamoja na kuwapa msaada wa vitu mbali mbali. Nawashukuru wale wote walioungana na mimi. Mungu awabariki sana" alisema Kajuna.
DSC_0236
 Mmiliki wa Kajunason Blog, Cathbert Angelo Kajuna akiwagawia juisi watoto yatima wakati wa kusherekea siku yake ya kuzaliwa kwenye  kituo cha kulelea  watoto yatima cha kituo cha SOS Children's Village Tanzania.
DSC_0263
Mmiliki wa Kajunason Blog, Cathbert Angelo Kajuna pamoja na mwenyekiti wa Tanzania Blogger Network (TBN) na mmiliki wa Blog ya The Habari Bw. Joachimu Mushi wakiwa kwenye pozi na watoto. Mwenyekiti wa TBN ni mmoja ya wageni waalikwa waliosindikiza.
DSC_0312
Cathbert Angelo Kajuna kiimbiwa wimbo na familia yake pamoja na baadhi ya watoto yatima wakati wa ukataji keki aliyokula na watoto hao katika kituo cha ha SOS Children's Village Tanzania kilichopo Karibu na kituo cha mabasi cha mawasiliano (SIMU 2000) jijini Dar.
DSC_0322
DSC_0325
DSC_0327
Cathbert Angelo Kajuna akiwalisha baadhi ya watoto yatima siku yake ya kuzaliwa kwenye  kituo cha SOS Children's Village Tanzania kilichopo Karibu na kituo cha mabasi cha mawasiliano (SIMU 2000) jijini Dar
DSC_0335
Cathbert Angelo Kajuna akimlisha keki rafiki yake Imani Ntila.
DSC_0336
Mmiliki wa Kajunason Blog, Cathbert Angelo Kajuna akimlisha keki mwenyekiti wa Tanzania Blogger Network (TBN) na mmiliki wa Blog ya The Habari Bw. Joachimu Mushi.
DSC_0337
Cathbert Angelo Kajuna akimlisha keki mwakilishi wa kituo cha SOS Children's Village Tanzania Bi. Sherry Mavura.
DSC_0347
DSC_0351
Watoto wakipewa zawadi.
DSC_0363
Picha ya pamoja.

No comments:

Post a Comment

Contact Form

Name

Email *

Message *

Tuwasiliane

Name

Email *

Message *