Mkuu
wa Mauzo na Masoko wa kampuni ya G4S, Alfred Elia, (katikati),
akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam
leo Machi 14, 2016 kuhusu ushirikiano baina ya kampuni yake na taasisi
ya kujitolea ya Uingereza ya Bhubesi Pride Foundation, (BPF), ambapo
taasisi hiyo inaendesha mafunzo ya kuunyanyua mchezo wa Raga (Rugby),
pamoja na kusaidia
jamii pamoja na maendeleo mashuleni na kwenye vituo vya kijamii. Shule
sita sita za jijini Dar es Salaam zitashindana katika mchezo huo
Jumamosi hii jijini. Wengine pichani, ni Meneja mradi wa BPF, Mark Cole,
(kulia) na Mkuu wa masuala ya fedha wa G4S, Paul Fullers.Mkutano huo na
waandishi wa habari ulifanyika jana Machi 14, 2016 (Picha K-VIS
EMDIA/Khalfan Said).
NA K-VIS MEDIA/Khalfan Said
TAASISI ya kujitolea ya Uingereza ya Bhubesi Pride Foundation (BPF)
kwa kushirikiana na kampuni ya ulinzi ya G4S ya jijini Dar es Salaam,
inaendesha mpango wa kuunyanyua na kuuendeleza mchezo wa Raga, (Rugby),
kusaidia jamii pamoja na maendeleo mashuleni na kwenye vituo vya
kijamii.
Akizungumza
kwenye mkutano na waandishi wa habari makao makuu ya G4S barabara ya
Ali Hassan Mwinyi jijini Dar es Salaam leo Machi 14, 2016, Mkuu wa
kitengo cha Mauzo na Masoko cha G4S, Alfred Elia, amesema, tayari
mafunzo hayo yamefanyika jijini Arusha na sasa yako hapa jijini Dar es
Salaam na yameanza rasminleo Jumatatu Machi 14, 2016 ambapo jumla ya
shule sita za msingi ziko kwenye mpango huo.
Amezitaja shule hizo kuwa ni pamoja na shule ya msingi, Mapambano, Makumbusho, Hananasifu, Victoria, Mugabe na Shekilango.
Kwa
upande wake, Meneja wa BPF, Mark Cole, alisema, mpango huo unaendeshwa
kwenye nchi mbalimbai za Afrika na ni wa mwaka mmoja. “Tayari tumefanya
mafunzo haya nchini Uganda, Kenya, Tanzania, Msumbiji, Malawi, Zambia,
Botswana, Namibia na Afrika Kusini, alisema Cole
Alisema,
nia ya mpango huo ni kuunganisha jamii kupitia raga, kuelimisha thamani
na stadi za maisha, pamoja na kunyanyua uwezo wa walimu nchini, kulea
viongozi wa jamii, wake kwa waume pamoja na kuweka uwezeshaji huu kuwa
endelevu.
Maendeleo
ya matokeo ya muda mrefu kupitia miradi inayoonekana, mfano kupanda
miti, kwa kushirikiana na wabia wetu katika nchi tajwa.
Tayari
shirika hili kwa kushirikiana na G4S Tanzania limeishafanya haya Arusha
na Moshi ambapo watoto zaidi ya watoto 600 wa mikoa hio walipata
mafunzo ya raga pamoja na stadi za maisha ambapo pia G4S ilipanda miti
katika maeneno mbalimbali
Naye
Mkuu wa masuala ya fedha wa G4S, Paul Fullers, alisema, G4S kwa
kutambua masuala ya usalama, ndio maana imeamua kushirikiana na BPF ili
kujenga uelewa miongoni mwa wanafunzi kuhusu masuala ya usalama wawapo
shuleni, mabarabarani na hata nyumbani.
“Mafundisho
haya yanafanyika kila mwaka kuanzia mwezi January mpaka Julai, ambapo
shuguli za kijamii hufanyika sambamba na makampuni yanayojitolea
kudhamini- G4S Africa, akiwa ni mdhamini mkuu na muhimu kwa hii
taasisi.” Alifafanua Fullers.
Mashirika
yasiyo ya kiserikali (NGOs). Vyama vya raga kitaifa, idara mbalimbali
za kiserikali, shule za kimataifa pamoja na makampuni mbalimbali kwenye
jamii husika, kuongezea thamani katika huu uhusiano pamoja na kujengea
uwezo, alisema.
Mark Cole, Meneja mradi wa BPF
Finn Sims, Meneja anayehusika na vyombo vya habari wa BPF
Paul Fullers, Mkuu wa masuala ya fedha wa G4S
Mkutano na wahanhabari ukiendelea
Wanahabari wakisikiliza kilichokuwa kikizungumzwa
Alfred Elia, akiwatambulisha wageni wake
No comments:
Post a Comment