Afya zetu : Dk. Bingwa wa Magonjwa ya Moyo, kuendesha huduma ya uchunguzi wa maradhi ya moyo Mkoani Kigoma - Wazalendo 25 Blog

Habari Mpya

Glory to Story.


Post Top Ad


25 Mar 2016

Afya zetu : Dk. Bingwa wa Magonjwa ya Moyo, kuendesha huduma ya uchunguzi wa maradhi ya moyo Mkoani Kigoma


 DAKTARI bingwa wa magonjwa ya moyo, Dkt. Stephan P. Masatu

NA K-VIS MEDIA/Khalfan Said
WATU wanaosumbuliwa na maradhi ya Moyo mkoani Kigoma, watapata faraja kubwa mapema Aprili 4 hadi 9, 2016,  kufuatia uwepo wa huduma za uchunguzi wa maradhi hayo utakaofanywa na Daktari Bingwa wa magonjwa ya Moyo, Dkt. Stephan P. Masatu, kutoka jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi jijini Dar es Salaam, Dkt. Masatu alisema, huduma zote za magonjwa ya moyo ikiwa ni pamoja na vipimo vya ECG na ECHO  zitatolewa kuanzia asubuhi kwenye hospitali ya kibinafsi ya Upendo iliyo jirani na soko kuu la mkoani Kigoma.
Mkoa wa Kigoma ni miongoni mwa mikoa iliyo pembezoni mwa nchi na zinakabiliwa na upungufu wa wataalamu wa kushughulikia magonjwa kama ya Moyo na kutokana na uchache wa wataalamu hao, itakuwa ni nafasi nzuri kwa wananchi wa mkoa huo pamoja na vitongoji vyake, kujitokeza ili kuhudumiwa ambapo kliniki hiyo itadumu kwa muda wa siku sita mfululizo.


 Dkt. Masatu akitumia mashine ya kupima ECHO, mmoja wa wagonjwa wa moyo

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad