Teknolojia :TCRA Yatoa Semina kwa Waandishi wa Habari Kugundua Simu Feki Zanzibar - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Wednesday, 3 February 2016

demo-image

Teknolojia :TCRA Yatoa Semina kwa Waandishi wa Habari Kugundua Simu Feki Zanzibar


DSC_0550
Meneja Mawasiliano wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania TCRA Innocent Mungy, akizungumza na waandishi wa habari Zanzibar kuhusiana na kutambua Simu Feki na kudhibiti uingiaji wa Simu hizo Tanzania na kueleza mwisho wa matumizi wa simu hizo Nchini Tanzania ni Juni 2016. Mkutano huo umefanyika katika ukumbi wa hoteli ya Zanzibar Ocean View Kilima Zanzibar na kuwashirikisha waandishi wa Vyombo mbali mbali vilioko Zanzibar. 
DSC_0571
Naibu Mkurugenzi Masuala ya Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano  TCRA Thadayo Ringo, akizungumza na waandishi wa habari jinsi ya kutambua Simu feki wakati wa mkutano huo na waandishi wa habari Zanzibar uliofanyika katika ukumbi wa hoteli ya Zanzibar Ocean View Kilimani Zanzibar, Amesema utambuzi wa kujua simu yako kama ni orijinali  unaweza kupiga namba kuaza na Nyota Reli 06 Reli . *# 06#  na utapata ujumbe wa Simu yako kwa Mfano zitakuja tarakimu 15  mfano   IMEI 12456789067654  Na Kupiga 15090 Ujumbe wa kukuelewesha kama ni simu yako orijino. kwa mfano kama huu Sony Mobile Communications AB -SONY  C5555 - Xperia. huu ni mfano wa kujua simu orijino.
DSC_0593
Naibu Mkurugenzi Masuala ya Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano Thadayo Ringo akionesha mfano wa simu orijino kwa waandishi wa habari wakati wa mkutano huo uliofanyika katika ukumbi wa hoteli ya Zanzibar Ocean View Kilimani Zanzibar.
DSC_0553
Waandishi wa habari wakifuatilia mkutano huo wa TCRA uliofanyika katika ukumbi wa hoteli ya Zanzibar Ocean View Kilimani Zanzibar.
DSC_0555
Waandishi wa habari wakifuatilia mkutano huo wa TCRA uliofanyika katika ukumbi wa hoteli ya Zanzibar Ocean View Kilimani Zanzibar.
DSC_0568
Waandishi wakifuatilia mafunzo hayo kwa vitendo kuangalia somu zao kama ni orijino baada ya kupata elimu hiyo ya kujua simu feki na orijino wakati wa mkutano huo na Maofisa wa TCRA uliofanyika katika ukumbi wa hoteli ya zanzibar ocean view kilimani zanzibar. kwa kuingiza namba waliopewa.
DSC_0585
Meneja wa Mawasiliano wa Mamlaka ya TCRA Innocent Mungy, akitowa maelezo kwa waandishi wa habari baada ya kuangalia simu zao baada ya kuingiza namba hizo na kugunduwa kuwa ziko salama na siyo feki. kwa bahati nzuri takribani waandishi wote simu zao orijino.
DSC_0588
Naibu Mkurugenzi Masuala ya Watumiaji Huduma za Maweasiliano Thadayo Ringo akimsomea ujumbe mmoja wa waandishi wa habari aliyehudhuria mkutano huo baada ya kuweka namba hizo na kuja ujumbe wa suimu siyo feki.
DSC_0595
Mdau wa habari Farouk Karim akiuliza swali wakati wa mkutano huo kuhusiana na uingiaji wa simu za kutoka ulaya nyingi huwa na lock wakati wa mkutano huo.
DSC_0599
Mwandishi Amour Mussa akiuliza kuhusu TCRA inachukua hatua gani endapo simu ikiibiwa.
DSC_0613
Ndg Issa Yussuf akuliza jinsi ya utaratibu wa kuwafikia Wananchi wa Vijiji na zoezi hilo la ungunduzi wa simu feki na kuweza kuepuka na hasara hii, wakati ikifika tarehe hiyo ya mwisho wa matumizi ya simu hizo feki. 
DSC_0603
Naibu Mkurugenzi Thadayo Ringo akifafanua na kujibu maswali yalioulizwa wakati wa mkutano huo na waandishi wa habari Zanzibar kuhusiana na matumizi ya Simu feki kufikia mwisho wake wa matumizi Tanzania.
DSC_0611
Meneja Mawasiliano TCRA  Innocent Mungy  akifafanua jambo wakati wa mkutano wao na waandishi wa habari Zanzibar kuhusiana na kusitishwa kwa matumizi ya simu feki ifikapo mwezi juni 2016. 
DSC_0616
Kaimu Meneja Mamlaka ya Mawasiliano Kanda ya Zanzibar TCRA Ndg Seif  S Waziri akizungumza wakati wa mkutano huo na kutowa neno la shukrani kwa waandishi wa habari kuhudhuria mkutano huo wa kutowa elimu ya simu feki kwa Wananchi wa Zanzibar na Tanzania uliofanyika katika ukumbi wa hoteli ya Zanzibar Ocean View Kilimani Zanzibar   
DSC_0562

DSC_0559
Waandishi wa habari wakifuatilia kwa makini mkutano huo wa mafunzo ya kutambua simu feki na Orijino uliofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Zanzibar Ocean View Kilimani Zanzibar.
Imetayarishwa na Othman Mapara.Blogspot.
Zanzinews.com. 

No comments:

Post a Comment

Tuwasiliane

Name

Email *

Message *

Contact Form

Name

Email *

Message *