Teknolojia :Mtambue kijana wa Kitanzania Desmond Andrew aliyeanzisha kampuni ya mawasiliano ya CW Net - Wazalendo 25 Blog

Habari Mpya

Glory to Story.


Post Top Ad


26 Feb 2016

Teknolojia :Mtambue kijana wa Kitanzania Desmond Andrew aliyeanzisha kampuni ya mawasiliano ya CW Net


Kijana wa Kitanzania Desmond Andrew alimeanzisha kampuni ya Mawasiliano ya CW Net  ambayo inatengeneza Power Bank, Smart Bracelet na Modem. Hakika Tanzania kuna vijana wengi kama Desmond Andrew lakini tatizo kubwa linalowakabili ni upatikanaji wa mtaji wa kuendeleaza vipaji vyao.
Mwanzilishi na mmiliki wa Kampuni ya Mawasiliano ya CW Net akimtoa ufafanuzi Mkurugenzi Mtendaji wa TPSF, Geoffrey Simbeye (aliyevaa suti) kuhusu Smart Bracelet na kazi zake katika maonesho yaliyoandaliwa na shirika la Viwango nchini Tanzania(TBS) yanayoendelea katika ukumbi wa Mlimani Cityjijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa TPSF, Geoffrey Simbeye (aliyevaa suti) akiuliza swali mara alipotembelea banda la CW Net maonesho ya Makampuni ya Kitanzania yanayotoa bidhaa yenye viwango vya kutosha hapa nchini.
Smart Bracelet hiki ni kifaa mojawapo kinachotengenezwa na kampuni ya Mawasiliano ya CW Net ambacho kifaa hicho kinahesabu hatua ambazo mtu ametembea nani kwa kiasi gani nguvu uliyoitumia pamoja na kukontrol muda unaolala na unaoamka, pia pia kifaa hicho kinaweza kuunganishwa na simu ya smartphone yako na kutambua simu ikiwa inaita kwa umbali wa mita kumi(10)
Hakika penda cha nyumbani

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad