![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEj6kkvLboAd6NuT4DyRHWhp4aHmHdfIA-Qne6uIKk8v8A3y8jYkDmKXvOgd5dbljVQWIZbbXTn6un7GpFKrm_X62obwIxnWvMMTTbv1FMKLhoTNUz79lbjLChULIXyPyg15qQPFrJg8aOQQ/s640/2.jpg)
Mkurugenzi
wa huduma ya Airtel Money Bw, Aijaz khan wakipongezana na Mkurugenzi wa
Biashara wa Total Bw, Romee De Villeneve mara baada ya kuingia ubia na
kuzindua Rasmi kadi maalum ya Airtel Money Tap Tap kwaajili ya kufanyia
malipo ya bidhaa mbalimbali katika vituo vya TOTAL. anaeshudia kulia ni
Meneja wa Biashara Total Bi Maria Lebby. Airtel imezindua kadi hiyo jana
ili kupunguza wimbi la wateja na watumiaji wa Airtel Money kutembea na
pesa taslim kwaajili ya usalama wao pia kuwawezesha kufanya malipo hata
kama simu zimezima.
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiNXZFi4AN7Z4COIcQiAD9_i_mP5pLK-lG2Ox5B4wsSGQXYs5OMWHBMnteg2ucUIuVITeae_FAOzTtcXgN1UhqHZyzfvjer_9rU_RK8tBMKmdDoDIXtAadgDAwlBVYpQ2tdjp0pqzC81eUy/s640/3.jpg)
Mkurugenzi
wa huduma ya Airtel Money Bw, Aijaz khan wakionyesha kadi na kifaa cha
malipo cha Tap Tap na Mkurugenzi wa Biashara wa Total Bw, Romee De
Villeneve mara baada ya kuingia ubia na kuzindua Rasmi kadi maalum ya
Airtel Money Tap Tap kwaajili ya kufanyia malipo ya bidhaa mbalimbali
katika vituo vya TOTAL. alieshikilia kifaa cha malipo cha Airtel Tap
tap kulia ni Meneja wa Biashara Total Bi Maria Lebby. Airtel imezindua
kadi hiyo jana ili kupunguza wimbi la wateja na watumiaji wa Airtel
Money kutembea na pesa taslim kwaajili ya usalama wao pia kuwawezesha
kufanya malipo hata kama simu zimezima.
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhsgO5yezTComROtDSDGLAnRmKThW4UWOK2TaqTLRs-dVLBEO0m5LVvnLEEnxxjB2Voop_V4qNbKXfqrkP3779FRQ6CFoh_kBvCp-sYI4YqjwgOzfo3_kt3b0eJ1SoymfxWfP080-RIKxdo/s640/4.jpg)
Mmoja
wa watangaziji mahiri wa kituo cha EFM redio Gadner G Habash akitumia
kadi ya kwanza kutolewa mara baada ya Airtel na Total kuingia ubia na
kuzindua Rasmi kadi maalum ya Airtel Money Tap Tap kwaajili ya kufanyia
malipo ya bidhaa mbalimbali katika vituo vya TOTAL. anaemuhudumia mtoa
huduma wa Total Bi Saumu Othmani (kati) na Meneja wa Airtel Money Bw,
Asupya Nalingigwa. Airtel imezindua kadi hiyo jana ili kupunguza wimbi
la wateja na watumiaji wa Airtel Money kutembea na pesa taslim kwaajili
ya usalama wao pia kuwawezesha kufanya malipo hata kama simu zimezima.
Kampuni
ya simu za mkononi ya imeingia ubia wa kibiashara na kampuni ya
kimataifa nchini ya TOTAL inayojihusisha na kuuza mafuta ya magari
pamoja na bidhaa za vilainisha ingini na mitambo, Ushirika huo wa Airtel
wa Total ni kupitia huduma ya kifedha ya Airtel Money wenye lengo la
kuwawezesha wateja wao kutumia kadi ya kugusisha ijulikanayo kama
‘AIRTEL MONEY TAP TAP’ kufanyia malipo yabidhaa katika vituo vyote vya
Total .
Kadi
ya Airtel Money ya Tap tap imeunganishwa moja kwa moja na akaunti ya
Airtel money ya mteja ili mteja aweze kuitumia mahali popote anaponunua
bidhaa yoyote katika vituo vya Total nchini. Kutokana na ushirika huo
wateja wote wa Airtel na Total watafurahia kupata huduma zote kwa
usalama zaidi bila kulazimika kubeba pesa taslimu.
Huduma
hii ya kadi ya malipo kwa kugusisha ya Airtel Money Tap tap imetokana
na ugunduzi wa utafiti wenye dhamira ya kuendelea kutumia teknolojia za
kisasa ili kuwezesha wateja kufanya malipo kwa urahisi na usalama zaidi.
Mteja atagusisha kadi tu kwenye kifaa maalumu cha kufanyia malipo na
kulipa papo hapo baada tu ya kuingiza namba yake ya siri ya Airtel
Money, teknolojia hiyo inajulikana kwa lugha ya kiingereza kama (Near
Field Communication).
Akiongea
wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo Meneja wa Huduma ya Airtel Money Tap
tap hiyo Bw, Stephen Kimea alisema “tunajisikia fahari sana leo kuingia
ubia na Total ili kuwaweze wateja wetu kufaidi kutumia huduma ya Airtel
Money Tap tap. Hii ni huduma yakwanza kutolewa nchini Tanzania na Airtel
ili kuboresha usalama zaidi kwa wateja pale wanapofanya malipo ya
huduma na bidhaa mbalimbali. Kila kwenye kituo cha Total wateja wetu
wataweza kutumia kadi hii, lengo letu ni kufanya wateja wetu wafurahie
huduma zetu zaidi”.
Kimea
aliendelea kueleza “Airtel tutahakikisha kuwa huduma hii ya kufanya
malipo kwa kutumia kadi ya Airtel Tap tap inapatikana kwa
wafanyabiashara na watoa huduma wakubwa na wakati zaidi ya elfu 25
nchini, hii nikutaka kutoa suluhisho la usalama wa raia kwa kuondokana
na tatizo la kubeba pesa nyingi wanapokwenda kufanya manunuzi na badala
yake sasa watatumia kadi hii”
“sasa
kadi hizi zitapatikana katika vituo vyote vya mafuta vya Total na
katika baadhi maduka yaliyo na nembo ya Airtel Tap Tap hapa nchini,
tunaamini huu ni mwendelezo wa kuboresha mfumo wa uhakika wa malipo kwa
teknolojia inayoendana na sasa” alimaliza kwa kusema Kimea.
Kwa
upande wake Mkurugenzi wa Biashara wa Total Nchini, Romee DE VILLENEUVE
alisema “Total tunazaidi ya vituo vya mafuta 30 nchini, hivyo basi
tunawahakikishia wateja wetu wote kupata huduma ya uhakika kila
watakapotembelea vituo vyetu vyote na kununua mafuta au kupata huduma
yoyote kwa kutumia kadi hizi za Airtel Money Tap tap. Tumeona umuhimu
kuboresha mfumo wetu wa malipo kwaajili ya kuwapa wateja urahisi na
usalama zaidi katika vituo vyetu, Tunaishukuru sana Airtel kwa kutuletea
teknolojia hii ya kisasa ya mfumo kufanya malipo kwa kadi yaAirtel
Money Tap tap”.
Huduma
ya Airtel Money Tap tap imeanza kutumika kwanza jijini Dar es salaam
kwa sasa na baadae itasambazwa nchi nzima katika vituo vyote vya Total
No comments:
Post a Comment