Kamishna
wa Fedha na Utawala wa Jeshi la Magereza, Gaston Sanga akisalimiana na
Kaimu Mkuu wa Chuo cha Ulinzi wa Taifa, Bregedia Jenerali, Jairos
Mwaseba alipotembelea Makao Makuu ya Jeshi la Magereza, Jijini Dar es
Salaam akiwa pamoja na Washiriki wa Mafunzo katika chuo hicho cha Ulinzi
wa Taifa(hawapo pichani) Februari 5, 2016(kushoto) ni Kamishna wa
Sheria na Uendeshaji wa Magereza, Dkt. Juma Malewa.
Kamishna
Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja akisalimiana na
Mkufunzi wa Chuo cha Ulinzi wa Taifa ambaye ni raia kutoka
China(katikati) ni Kaimu Mkuu wa Chuo cha Ulinzi wa Taifa, Bregedia
Jenerali, Jairos Mwaseba alipotembelea Makao Makuu ya Jeshi la Magereza,
Jijini Dar es Salaam akiwa pamoja na Washiriki wa Mafunzo katika chuo
hicho cha Ulinzi wa Taifa(hawapo pichani) Februari 5, 2016.
Kamishna
Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja akiongea na Ujumbe
kutoka Chuo cha Ulinzi wa Taifa(hawapo pichani). Ujumbe huo wa Washiriki
wa Mafunzo wametembelea Ofisi za Makao Makuu ya Jeshi la Magereza
katika ziara yao ya Mafunzo kuhusu Uendeshaji wa shughuli za Magereza
hapa nchini.
Wakunzi
wa Chuo cha Ulinzi wa Taifa wakifuatilia kwa makini mazungumzo kati yao
na Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja(hayupo
pichani). Kushoto ni Kaimu Mkuu wa Chuo cha Ulinzi wa Taifa, Bregedia
Jenerali, Jairos Mwaseba.
Kamishna
wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza, Dkt. Juma Malewa akitoa maelezo
mafupi kwa Washiriki wa Mafunzo kutoka Chuo cha Ulinzi wa Taifa
walipotembelea Kiwanda cha Gereza Kuu Ukonga kwa ziara yao ya
Mafunzo(kushoto) ni Mkuu wa Magereza Mkoa wa Dar es Salaam, Kamishna
Mwandamizi wa Magereza, Augustine Mboje.
Baadhi
ya Washiriki wa Mafunzo kutoka chuo cha Ulinzi wa Taifa wakImwangalia
mmoja wa wafungwa ambaye amepatiwa ujuzi gerezani wa kukata vitambaa vya
nguo tayari kwa kushona nguo za wafungwa wliopo magerezani kama
anavyoonekana katika picha katika Kiwanda cha Gereza Kuu Ukonga, Jijini
Dar es Salaam.
Kaimu
Mkuu wa Chuo cha Ulinzi wa Taifa, Bregedia Jenerali, Jairos
Mwaseba(katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Wahiriki wa
Mafunzo(waliosimama mstari wa nyuma) walipotembelea Jeshi la Magereza
kujifunza uendeshaji wa Jeshi hilo(wa nne kushoto) ni Kamishna wa Sheria
na Uendeshaji wa Magereza, Dkt. Juma Malewa.(Picha zote na Lucas Mboje
wa Jeshi la Magereza).
No comments:
Post a Comment