Asteria Muhozya na Rhoda James, Mbinga.
Serikali imesema itahakikisha inafanya Makaa ya Mawe yanakuwa chanzo kingine kikubwa cha uzalishaji umeme Nchini.
Hayo
yameelezwa na Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo
alipotembelea Mgodi wa Makaa ya Mawe wa Ngaka unaomilikiwa kwa ubia
Kati ya Kampuni ya TANCOAL na Serikali kupitia shirika la NDC. Mgodi
huo upo katika Wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma.
Aidha,
ili kufikia lengo hilo ,Prof. Muhongo amesema Serikali itahakikisha
inafanya kazi kwa ushirikiano mkubwa na Mgodi huo ambao Serikali ina
umiliki wa hisa ya asilimia 30 kupitia Shirika la Maendeleo ya Taifa
(NDC) ili kuimarisha uchumi wa taifa kupitia Makaa ya Mawe.
Ameongeza
kuwa, ili kuhakikisha kwamba Kampuni ya TANCOAL inaendelea kuzalisha
makaa na kutumiwa na viwanda vya ndani, Prof Muhongo amevitaka viwanda
vilivyoingia Mkataba wa mauziano na mgodi huo kuacha kununua Makaa
kutoka nje ikiwa makaa ya Ngaka yanakidhi viwango na ubora unaotakiwa.
"Nimeelezwa
Makaa ya Ngaka yana ubora na kiwango cha hali ya juu na nimeelezwa
kwamba kuna baadhi ya viwanda vimeingia mkataba na Ngaka lakini badala
yake wananunua makaa kutoka nje. Hilo halikubaliki ikiwa makaa ya ndani
ya nchi yana ubora lazima tutumie bidhaa za nyumbani,"amesisitiza Prof.
Muhongo.
Kutokana
na malalamiko ya Mgodi kuhusu hali ya Mkataba ya kuuziana makaa
kutoafikiana, Waziri Muhongo ameutaka mgodi huo,NDC,EWURA, Kampuni za
Saruji za Dangote, Tanga Cement na Shirika la Umeme Nchini (TANESCO)
kukutana Makao Makuu ya Wizara tarehe 14 Januari,2016, ili kujadili
kuhusu suala hilo na pia kujadiliana juu ya gharama za kuuziana umeme
na TANESCO pindi mgodi huo utakapoanza kuzalisha umeme kwa kutumia makaa
ya mawe.
"
Umeme wa makaa ya mawe Tanzania ni lazima. Tutapigana kufa na kupona
kuhakikisha tunazalisha umeme kwa kutumia makaa ya mawe kwa sababu
gharama zake zitakuwa nafuu kwa wananchi na pia umeme huu utachochea
ukuaji wa viwanda nchini," amesisitiza Prof. Muhongo.
Kadhalika
Prof. Muhongo amerejea kauli yake ya kuwataka wazalishaji umeme hususan
wa makaa ya mawe na vyanzo vingine kuhakikisha wanaiuzia TANESCO umeme
wa bei ya chini na kuongeza "mauziano ya umeme wa makaa ya mawe lazima
yafuate viwango vya kimataifa. Lazima yawe ya gharama nafuu."
Katika
hatua nyingine, Prof. Muhongo amewataka EWURA kubadilika na kushiriki
katika hatua za mwanzo za majadiliano ya gharama za kuuziana umeme
katika utekelezaji wa miradi mbalimbali badala ya kusubiri kushiriki
katika hatua za mwisho na kulieleza jambo hilo kuwa ushiriki wao katika
hatua za awali unawezesha majadiliano na makubaliano kufanyika kwa
haraka.
Aidha,
Prof. Muhongo amechukua fursa hiyo kuzitaka Mamlaka chini ya wizara
kuzingatia suala la usawa na namna Serikali inavyonufaika na makubaliano
ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya kitaifa kwa kuzingatia kuwa
rasilimali ni za nchi , hivyo taifa linapaswa kunufaika na uwekezaji
husika.
Kwa
mujibu wa Mkuu wa Masoko wa mgodi wa Ngaka, Christopher Temba, mgodi huo
unazalisha tani za makaa ya mawe Laki Tano kwa mwaka lakini lengo ni
kufikia tani milioni moja.
Tayari
makaa hayo yanasafirishwa katika nchi za Kenya, Zambia, Malawi na
vilevile katika viwanda kadhaa hapa nchini vikiwemo vya Saruji Tanga
Mohamed Enterprises na viwanda vingine
Waziri
wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (katikati) akizungumza
na baadhi ya watendaji wa Mgodi wa Makaa ya Mawe ya Ngaka mara baada ya
kuwasili katika mgodi huo wakati wa ziara yake ya kikazi mkoa wa Ruvuma.
Wengine ni ujumbe aliofuatana nao pamoja na Mbunge wa Mbinga
vijijini, Martin Msuha, Mkuu wa Wilaya ya Mbinga Senyi Ngaga, Kamishna
Msaidizi wa Madini, anayeshughulikia Leseni John Nayopa, Watendaji toka
Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Shirika la Maendeleo ya Taifa
(NDC), Ofisi ya Madini Kanda ya Ziwa Nyasa, baadhi ya Maafisa toka
Wizara ya Nishati na Madini na EWURA.
Waziri
wa Nishati na Madini, Profesa Sospter Muhongo, (kulia) akiwasikiliza
wawakilishi wa wananchi wa Kijiji cha Mtundualo, Wilaya ya Mbinga ambao
walimwomba waziri asikilize malalamiko yao ikiwemo kuhusu suala la
fidia kupisha mradi wa Makaa ya Mawe wa Ngaka na ombi la kijiji hicho
kupatiwa umeme. Kwa mujibu wa Meneja wa Tanesco Kanda ya Kusini, Joyce
Ngahyoma, amewahakikishia kuwa ifikapo mwezi Aprili mwaka huu kijiji
hicho kitakuwa kimeunganishwa na nishati ya umeme.
Mkuu
wa Wilaya ya Mbinga Senyi Ngaga, akijadiliana jambo na baadhi ya
Watendaji wa Mgodi wa Ngaka kampuni ya TANCOAL, mara baada ya waziri
kukagua shughuli za mgodi huo na kusikia malalamiko ya wananchi kuhusu
fidia. Waziri Muhongo amezitaka pande mbili kati ya Kampuni, Halmashauri
na wananchi kukutana ili kujadili na kukubaliana kuhusu masuala kadhaa
yakiwemo fidia na uhifadhi wa mazingira.
Waziri
wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, akimsikiliza
Mwendeshaji Mitambo wa kituo cha kufua umeme cha Tulila kinachomilikiwa
na Shirika la Wabenedictin wa Mtakatifu Agnes Chipole, Sister Maria
Katani (OSB),. Wengine wanaofuatilia nia Meneja wa Tanesco Kanda ya
Kusini, Joyce Ngahyoma na Afisa toka Wizara ya Nishati na Madini,
Christopher Bitesirigwa.
Waziri
wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, akisalimiana na
Mfadhili wa Kituo cha Kufua umeme kinachomilikiwa na Watawa wa Shirika
la Shirika la Wabenedictin wa Mtakatifu Agnes Chipole, Albert Cock
(kushoto). Kituo hicho chenye uwezo wa kuzalisha kilowati 800 kipo Kata
ya Magarura, wilaya ya Mbinga mkoa wa Ruvuma. Aidha, sehemu ya umeme
unaozalishwa na kituo hicho unasambazwa Songea, JKT Mlale na Chuo cha
Maendeleo ya Jamii Mlale. Vilevile, Kituo hicho kipo katika hatua za
ujenzi wa kituo kitakachokuwa na uwezo wa kuzalisha megwati 7.5.
Meneja
wa Tanesco Kanda ya Kusini, Joyce Ngahyoma akimweleza jambo Waziri wa
Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo wakati alipotembelea kituo
cha mwekezaji binafsi cha Kufua umeme kinachomilikiwa na Familia ya
Andoya, Wilaya ya Mbinga. Mradi huo wa Mbangamao unazalisha megawati
0.2, huku malengo ni kufikia megawati 2. Anayemsikiliza nyuma yake ni
Meneja wa Tanesco Mkoa wa Ruvuma, Patric Lwesya, wengine ni ujumbe
uliofuatana na Waziri.
Waziri
wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo katika picha ya pamoja
na Watawa wa Shirika la Shirika la Wabenedictin wa Mtakatifu Agnes
Chipole, Mfadhili wa Kituo hicho cha kufua umeme Albert Cock, ujumbe
aliofuatana nao wakiwemo Maafisa toka Wizara ya Nishati na Madini,
EWURA, Shirika la Umeme Nchini, Shirika la Maendeleo ya Taifa (NDC),
Uongozi wa Wilaya ya Mbinga, Mbunge wa Mbinga Vijijini Martin Msuha,
Uongozi wa Kijiji, Wakandarasi wanaojenga kituo cha kuzalisha umeme cha
megawati 7.5, na baadhi ya wananchi wanaozunguka eneo hilo.
Baadhi
ya Maafisa Kutoka Wizara ya Nishati na Madini (Mbele) na ujumbe
uliofuatana na Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo
(nyuma) kutembelea kituo cha Kufua umeme cha Tulila kinachomilikiwa na
Watawa wa Shirika la Wabenedictin wa Mtakatifu Agnes Chipole,wakiangalia
maendeleo ya mradi wa ujenzi wa Bwawa la kufua umeme. Imeelezwa kuwa,
kukamilika kwake kutawezesha uzalishaji wa umeme wa kiasi cha megawati
7.5.
Waziri
wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, katika picha ya pamoja
na Watawa Shirika la Wabenedictin wa Mtakatifu Agnes Chipole na Mfadhili
wa Kituo hicho Albert Cock.
No comments:
Post a Comment