Afisa Uhusiano wa Jiji la Arusha, Bi. N'tegenjwa Hosea.
Na Vero Ignatus , Wazalendo 25 Blog - Arusha.
Wito umetolewa kwa wakazi wa jiji la Arusha na vijiji jirani kuwa makini na waepuke kula hovyo maeneo ambayo siyo masafi ambayo yatapelekea kuhathiri afya zao
Hayo yamesemwa na Afisa uhusiano wa Jiji la Arusha bi N'tegenjwa Hosea alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhisiana na mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu.
Aidha bi N'tegenjwa amesema kuwa kwenye kambi ya wagonjwa wa kipindupindu Levolosi jijini hapo imepokea wagonjwa10 ambapo waliolazwa wodini ni wagonjwa 5 ambapo jumla yao ni wagonjwa 15.
Ameainisha Kata walizotoka wagonjwa hao ni Kata ya Sinoni wagonjwa 2 ,Olasiti mgonjwa 1,Sokoiniwani wagonjwa 2 ,Ungalimitedi mgonjwa 1,nje ya mipaka ya jiji la Arusha. wamepokea mgonjwa kutoka Arusha Dc 1,Kata ya Sakina 1,Murieti 1na Sombetini mgonjwa 1.
Hivyo wananchi wote wametakiwa kuzingatia kanuni zote za usafi kwani hali ilivyo kwa sasa hairidhishi,na kila mmoja atambue kuwa jukumu la kuzingatia usafi ni la mtu binafsi ili kutokomeza kabisa ugonjwa huu wa kipindupindu.
No comments:
Post a Comment