Afya Zetu : Waziri Mkuu, Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa Atembelea Hospitali ya Mkoa wa Ruvuma - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633

Thursday, 7 January 2016

Afya Zetu : Waziri Mkuu, Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa Atembelea Hospitali ya Mkoa wa Ruvuma


  Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akizungumza na baadhi ya wananchi waliofika kuwahudumia wagonjwa wao waliolazwa kwenye hospitali ya mkoa wa Ruvuma baada ya kuitembelea akiwa katika ziara ya mkoa huo Januari 5, 2016.Kushoto ni Mkuu wa Mkoa huo, Thabiti Mwabungu na kulia ni Mbunge wa Songea Mjini, Leonidas Gama. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Thabiti  Mwambungu.

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa,akimsalimia mtoto Flora Mapunda (1) ambaye amelazwa katika hospitali ya Mkoa wa Ruvuma ambayo  Waziri Mkuu aliitembelea na  kuzungumza na watumishi  akiwa ktika ziara ya mkoa huo Januari 5, 2016.

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na bibi Antonia Moyo ambaye alikuwa akipata matibabu katika chumba maalum cha waze katika hospitali ya mkoa wa Ruvuma wakati alipoitembelea hositali hiyo akiwa katika ziara ya mkoa huo Januari 5, 2016. Kulia ni Mkuu wa Mkoa huo Thabiti Mwabungu.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimsalimia Josephine John  ambaye amelazwa katika hospitali ya mkoa wa Ruvuma kwa matibabu. Alikuwa katika ziara ya mkoa huo Januari5, 2016.
 Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akizungumza na Madaktari na Wauguzi wa Hospitali ya Mkoa wa Ruvuma baada ya kuitembelea akiwa katika ziara ya mkoa huo Januari 5, 2016.Kushoto ni Mkuu wa Mkoa huo, Thabiti Mwabungu na kulia ni Mbunge wa Songea Mjini, Leonidas Gama.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

No comments:

Post a Comment