Mbunge wa Monduli kupitia CHADEMA Julius Kalanga akikabidhiwa fimbo
maalum na mzee wa Mila maarufu kama Laigwanan ishara ya kupewa mamlaka
na uongozi katika ziara yake aliyoifanya jana katika eneo la Mto wa Mbu.
Mbunge wa Monduli kupitia CHADEMA Julius Kalanga akizungumza na wananchi katika eneo la Mto wa
Mbu.Kufuatia ziara yake ya kutembelea wananchi .Picha na Ferdinand Shayo
Na Ferdinand Shayo wa Wazalendo 25 Blog ,Monduli.
Wananchi
wilayani Monduli wametahadharishwa juu ya uuzaji holela wa ardhi ambao umekua
ukipelekea migogoro baina ya wananchi na wawekezaji jambo linaloathiri shughuli
za maendeleo .
Kufuatia
ziara ya Mbunge wa Jimbo hilo Julius Kalanga kwa mwekezaji Meno Safari kutoka
nchini Uholanzi ,mwekezaji huyo amekua akilalamikiwa na wananchi kumiliki
maeneo ya kilima ambacho kilikua kikitumika kwa ajili ya shughuli za malisho
,wananchi hao wamesema kuwa mwekezaji huyo amekuaepo kwa takribani nmiaka 10 na
bado hajaelewa shughuli za mwekezaji huyo na mchango wake katika jamii.
Wananchi hao
wameitaka serikali ichukue hatua juu ya mwekezaji huyo ambaye umiliki wake wa
maeoneo hayo unatiliwa mashaka na kuyarudisha maeneo hayo ambayo awali yalikua
maeneo ya malisho ya wafugaji.
Mbunge wa
Mondli Julius Kalanga akihutubia wananchi hao mara baada ya kukamilisha ziara
yake amewataka wananchi na watendaji kuwa makini na kuacha kugawa ardhi
kiholela kwani wanaweza kuwa chanzo cha migogoro na kuchochea uwekezaji usio na
tija unaolenga kunyonya rasilimali za nchi.
Wilaya ya
Monduli inategemea shughuli za ufugaji kama shughuli kuu za uchumi ,licha ya
ufugaji bado inakabiliwa na tatizo la uhaba wa maji ,migogoro ya ardhi na
miuondombinu isiyopitika hasa maeneo ya vijijini.
No comments:
Post a Comment