Mkurugenzi wa Jamii Media group ,Pamela Mollel akikabidhi msaada wa
mahitaji ya kibinadamu kwa wazee waishio kata ya Kimandolu jijini
Arusha ,anayepokea ni Mwenyekiti wa Baraza la wazee mtaa wa kimandolu Emmanuel
Mollel ,Kata ya Kimandolu ina jumla ya wazee 400 ambao
wanakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa huduma za afya,lishe duni na
huduma za kijamii.
Mkurugenzi wa Jamii Media group ,Pamela Mollel akifafanua jambo kwa wazee wazee waishio kata ya Kimandolu jijini Arusha alipofika kuwatembelea na kutoa msaada wa kibinadamu.Kata ya Kimandolu ina jumla ya wazee 400 ambao wanakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa huduma za afya,lishe duni na huduma za kijamii.Picha na Ferdinand Shayo
Mkurugenzi wa Jamii Media group ,Pamela Mollel akifafanua jambo kwa wazee wazee waishio kata ya Kimandolu jijini Arusha alipofika kuwatembelea na kutoa msaada wa kibinadamu.Kata ya Kimandolu ina jumla ya wazee 400 ambao wanakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa huduma za afya,lishe duni na huduma za kijamii.Picha na Ferdinand Shayo
Na Ferdinand Shayo wa Wazalendo 25 Blog,Arusha.
Wazee
waishio kata ya Kimandolu wilaya ya Arusha mkoani Arusha wamemuomba Rais John
Pombe Magufuli awakumbuke wazee kwa kuhakikisha kuwa wanapata huduma bora za
afya ,lishe bora na kupata mafao ya uzeeni kutokana na mchango wao katika
ujenzi wa taifa kupitia sekta binafsi na za serikali tangu nchi ipate uhuru.
Wazee hao
ambao wanaishi katika hali ngumu za kimaisha na wengine kutokua na uhakika wa milo
mitatu huku wakikabiliwa na jukumu la kulea familia zao pamoja na wajukuu licha
ya uzee unaowakabili pamoja na kutokua na kipato cha uhakika na wengine kutokua
na nguvu ya kufanya kazi.
Amon Mwita ni mzee anayeishi kata ya Kimandolu alisema
kuwa licha ya mchango wao katika uchumi
wa nchi na maendeleo ya taifa tangu kipindi cha uhuru wamekua ni watu wa
kusahaulika jambo ambalo linawafanya waiishi maisha ya shida.
Mwita alisema
kuwa kwa muda mrefu wamekua wakipigwa danadana juu ya kupatiwa matibabu bure
hali ambayo imesababisha afya za wazee wengi kuzoroto kwani wengine hukosa
fedha za matibabu na kujikuta wakipoteza maisha kwa kukosa matibabu.
Navoneiwa
Maeda ni mzee ameitaka Serikali
iwathamini wazee kwani ni kundi linaloishi katika mazingira magumu na bado
halijapewa kipaumbele na serikali jambo ambalo linawaumiza hivyo ameiomba
serikali na jamii ichukue jukumu la kuwalea wazee na kuwatunza.
Mwenyekiti
wa Baraza la wazee mtaa wa kimandolu Emmanuel Mollel asema kuwa wazee wengi
wamekua wakijificha majumbani ingali wagonjwa bila kupata matibabu na wengine
kutopata mlo wa siku kutokana na hali ngumu za kiuchumi walizonazo hivyo
ameiomba jamii ijitokeze kuwasaidia wazee.
Mkurugenzi
wa Jamii Media Group Pamela Mollel na Mdau wa wazee Amedeus Moshi waliofika kuwatembelea wazee hao na kutoa msaada wa kibinadamu wameitaka
jamii itambue wajibu wake wa kuwalinda na kuwatunza wazee pamoja na kukemea
mauaji ya vikongwe suala linalochafua taswira ya taifa na kuathiri ustawi wa
wazee nchini.
No comments:
Post a Comment