Jumapili iliyoisha ya tarehe 08.11. 2015, wanawake mbali mbali jijini Dar es salaam
walikutana katika tamasha la kitchen party gala likiwa limebeba ujumbe wa
mwanamke simama na timiza ndoto zako.
Wanawake
wakiwa wamevalia khanga ambayo ndio ilikuwa dress code ya tamasha walikusanyika
kwa wingi kwa ajili ya kupata mafunzo na ushauri bila kusahau burudani.
Pia Ilichezeshwa droo ya kushinda safari ya Afrika Kusini kwa siku mbili alishinda, iliyodhaminiwa na kinyago tours. Pamoja na droo ya kumtafuta Mshindi wa safari ya Mikumi national park nae alipatikana akapokea certificate toka kwa mkurugenzi wa kinyago tours bi Diana.
Pia Ilichezeshwa droo ya kushinda safari ya Afrika Kusini kwa siku mbili alishinda, iliyodhaminiwa na kinyago tours. Pamoja na droo ya kumtafuta Mshindi wa safari ya Mikumi national park nae alipatikana akapokea certificate toka kwa mkurugenzi wa kinyago tours bi Diana.
Pichani juu ni washiriki wa kitchen party gala wakifuatilia mafunzo kwa umakini.
Msemaji Bi Mariam Mbewa
Mkurugenzi wa green investment akielezea safari yake ya mafanikio na
kuwafundisha kinamama umuhimu wa kuweka akiba.
Pichani juu ni washiriki wa kitchen party gala wakifuatilia mafunzo kwa umakini huku wakiwa na furaha tele juu ya kile kinachoelezewa kutoka kwa Msemaji.
Msemaji Bi Maida Waziri mkurugenzi wa Ibra Contractors
nae alishirikisha wanawake safari yake ya mafanikio toka akiwa fundi cherehani
mpaka sasa anamiliki kampuni kubwa ya ujenzi wa majengo na bara
bara.Aliwasisitiza wanawake kujiamini na kutokuogopa kuthubutu ukijiamini
popote unapenya lakini lazima uwe na malengo na mikakati.
Mwalimu wa masuala ya biashara na ujasiriamali Bryson
Makena nae alitema cheche zake na kuwafundisha kina mama kujitambua na ujue
kusudio lao hapa duniani ni lipi.
Waandaaji wa women in balance kitchen party gala
Mtangazaji wa E fm Dina Marios na Vida Mndolwa wakigonga chears kufungua
shughuli.
Wadada wakifurahi
Muongoza shughuli Dina Marios akisisitiza jambo
Ilichezeshwa droo ya kushinda safari ya Afrika Kusini
kwa siku mbili na huyu dada ndio alishinda.Atasafiri na mumewe mtarajiwa na
imedhaminiwa na kinyago tours.
Mshindi wa safari ya Mikumi national park nae
alipatikana bi Edna Haki Ngowi akipokea certificate toka kwa mkurugenzi wa
kinyago tours bi Diana
Mchungaji debora akifundisha kina mama kuwa wao ni wasababishaji wanaweza kufanya mambo yasiyowezekana yakawezekana.
PICHA NA DINA MARIOS
No comments:
Post a Comment