Mwanamuziki
nyota nchini Tanzania, Nassib Abdul ama Diamond Platnumz akiongea na
waandishi wa habari (hawapo pichani). (Picha na Andrew Chale,
Modewjiblog).
Na Andrew Chale, Modewji.
KAMPUNI
ya MultiChoice Tanzania mapema jana imezindua ofa kabambe za msimu wa
siku kuu huku ikimtambulisha rasmi Mwanamuziki Diamond Platnumz kuwa
balozi maalum wa bidhaa za kampuni hiyo ikiwemo kifurushi cha DSTV
BOMBA chenye chaneli zaidi ya 65 ikiwemo huduma ya vituo kadhaa vya
televisheni za hapa nchini.
Akimtambulusha
rasmi Meneja Masoko wa kampuni hiyo, Furaha Samalu, amemtambulisha
Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ kuwa balozi wa king’amuzi hicho na
kutaja gharama zake kuwa ni shilingi 23,500/= kwa malipo ya mwezi na
king’amuzi chenyewe kinapatikana kwa shilingi 79,000/= na kuwataka
wananchi kuchangamkia huduma hiyo muhimu katika msimu huu wa ofa za
sikukuu.
Meneja
masoko huyo ameongeza kuwa, kifurushi hicho kimesambaa nchini
mbalimbali barani Afrika hivyo wasanii wa filamu, muziki na wengineo
ambao watang’aa kwenye vipindi hivyo watakuwa wakionekana pande
mbalimbali barani Afrika na hivyo kuwapatia umaarufu na kuwaongezea soko
la kazi zao.
Mwanamuziki
Diamond Platinumz akisoma kipeperushi chenye maelezo juu ya ofa
mbalimbali za DStv wakati wa utambulisho wa ofa za sikukuu pamoja na
kutangazwa kwa balozi huyo wa bidhaa za DSTV. Katikati Afisa Masoko wa
Multichoice Tanzania, Furaha Samalu na kushoto ni Meneja Mwendeshaji wa
Multichoice Tanzania, Ronald Baraka Shelukindo.
Meneja
Masoko wa Multichoice Tanzania, Furaha Samalu akifafanua jambo katika
mkutano huo na kushoto ni Meneja Mwendeshaji wa Multichoice Tanzania,
Ronald Baraka Shelukindo na upande wa kulia ni msanii Diamond Platnumz
balozi wa bidhaa za DSTV.
Meneja
mauzo wa DSTV, Bw. Salum Salum akifafanua jambo juu ya ofa hiyo mpya
na mahaala wanapopatikana nchini kwa mawakala wote ambapo amewaomba
watanzania kuchangamkia ofa ya kuunganishwa haraka huduma bora zaidi za
chaneli za kisasa kupitia DSTV.
Baadhi ya wanahabari wakifuatilia mkutano huo wa DSTV..
Mwandishi wa gazeti la Raia Tanzania akiuliza swali juu ya bidhaa za DSTV..
Mpiga picha wa Magazeti ya Habari leo, Fadhili Akida akiuliza swali katika mkutano huo wa DSTV..
Ilifika wakati wa zawadi.. Diamond akisoma jina la mwandishi wa habari aliyeshinda zawadi hiyo..
Diamond
Platnumz akimkabidhi mwandishi wa habari, Sangu Joseph king'amuzi
alichojishindia katika droo iliyochezeshwa wakati wa mkutano huo.
Diamond akikabidhi zawadi ya King'amuzi cha DSTV kwa mwandishi wa habari Rajab Musa baada ya kushinda..
Diamond akikabidhi zawadi ya king'amuzi kwa mwandishi wa habari, Joseph Mchekadone baada ya kushinda..
Diamond Platnumz akimkabidhi king'amuzi mwanahabari wa ITV, Ester Sangai baada ya kuibuka mshindi..
Meneja
mauzo wa DSTV, Bw. Salum akisisitiza juu ya ofa hiyo ambapo ameeleza
kuwa wateja watapa kujionea chaneli mbalimbali zenye mvuto na picha za
kuvutia huku bidhaa zake zikiwa ni tofauti kabisa na zingine.
No comments:
Post a Comment