Mfuko wa Jamii : Radio 5 Yawaunganisha PSPF na wadau wake - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

Sunday, 29 November 2015

Mfuko wa Jamii : Radio 5 Yawaunganisha PSPF na wadau wake

Wapili kushoto ni Mkurugenzi mkuu wa mfuko wa kijamii wa PSPF Adam Mayingu ,kulia ni Afisa mahusiano wa mfuko huo Bw.Abdul Njaidi akifatiwa na meneja Masoko na Mahusiano wa Radio 5 Bi.Sarah Keiya pamoja na Meneja Biashara wa kituo hicho Bi.Angela Maina
Na Mwandishi Wetu,

Kampuni ya Tana Communication Media inayomiliki kituo cha Radio 5  pamoja na mfuko wa kijamii wa PSPF imewafikia wadau wa mfuko huo kwa kuwapa elimu kupitia kipindi cha “Good-Morning Tanzania

Mkurugenzi mkuu wa mfuko huo Bw.Adam Mayingu akiongozana na Afisa mahusiano wa mfuko huo Bw.Abdul Njaidi walipokelewa na meneja Masoko na Mahusiano wa Radio 5 Bi.Sarah Keiya pamoja na Meneja Biashara wa kituo hicho Bi.Angela Maina

Akizungumza katika kipindi hicho kinachorushwa na kituo hicho Bw.Adam alisema kuwa ni wajibu wao kutoa elimu kwa jamii ili iweze kupata fursa ya kufahamu vema mfuko huo pamoja na kufaidika na huduma za afya za PSPF kupitia NHIF

Kwa upande wake Meneja masoko na mahusiano wa Radio 5 Bi.Sarah alisema uwepo wa mifuko ya kijamii inawezesha wananchi kupanga maisha yao ya sasa na baadae  na ndio maana Radio 5 imekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha mipango ya mifuko hii inawafikia walengwa

Bi,Sarah alisema kuwa Mkurugenzi wao Bw.Robert Francis amekuwa akiwezesha idara yao ya masoko na biashara kwa kutoa bei nafuu ya matangazo kwa mifuko hii ya kijamii ili kuwezesha kuwafikia wananchi kwa wingi na urahisi

No comments:

Post a Comment