Wananchi
wa Kijiji cha Igamba ambao ni wakulima wa Kahawa wakipiga picha ya
pamoja baada ya kupata elimu na kujiunga na NSSF kama wanachama wa Hiari
chini ya Mpango wa Wakulima Scheme ambao utawasaidia Kupata Matibabu
bure na Kujipatia Mikopo ya pembejeo.
Maafisa
wa NSSF mkoa wa Mbeya wakiwaandikisha watu kutoka Sekta binafsi
waliokusanyika kwenye kituo cha mabasi cha mbalizi kwenye kampeni maalum
ya NSSF ya kutoa elimu na kuandikisha wanachama Mkoani mbeya ili
kuongeza wigo wa wanachama.
Meneja
wa NSSF Mkoa wa mbeya, Robert Kadege akimsaidia mmoja wa Madereva wa
Bodaboda kujaza fomu ya NSSF kwa ajili ya Kumuandikisha kujiunga na
NSSF.
Meneja
Kiongozi Masoko na uhusiano wa NSSF Eunice Chiume na Meneja wa Mkoa wa
Mbeya Robert Kadege wakitoa elimu kwa dereva wa daladala mkoani Mbeya
kwenye kampeni maalumu ijulikanayo kama NSSF Kwanza iliyolenga kuwafikia
watu walio kwenye sekta binafsi ili wajiunge na NSSF.
Wananchi:
Wananchi wa Mkoa wa Mbeya wakiwa wamekusanyika kwenye banda la NSSF ili
kupata elimu na kujiandikisha na Mfuko huo eneo la stendi ya Magari ya
Mbalizi Mkoani Mbeya.
No comments:
Post a Comment