Mazingira Yetu : Jumuiko la Maliasili Tanzania (TNRF) Wamtaka Magufuli Adhibiti Upotevu wa Maliasili Tanzania - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633

Friday, 6 November 2015

Mazingira Yetu : Jumuiko la Maliasili Tanzania (TNRF) Wamtaka Magufuli Adhibiti Upotevu wa Maliasili Tanzania

Mwenyekiti wa Bodi ya Jumuiko la Maliasili nchini (TNRF) ,Dr.Suma Kaare akizungumza katika mkutano wa 7 wa jumuiko hilo uliofanyika jijini Arusha na kuhudhuriwa na mashirika binafsi pamoja na washiriki kutoka wizara mbalimbali. Picha na Gadiola Emmanuel
  Mratibu wa mradi wa Mabadiliko ya Tabia nchi unaofadhiliwa na IIED Bw. Alais Morindat akifafanua jambo  katika mkutano wa 7 wa jumuiko hilo uliofanyika jijini Arusha na kuhudhuriwa na mashirika binafsi pamoja na washiriki kutoka wizara mbalimbali.Picha na Gadiola Emmanuel
  Mkurugenzi wa Shirika la AWF ,John Salehe  akifafanua jambo  katika mkutano wa 7 wa jumuiko hilo uliofanyika jijini Arusha na kuhudhuriwa na mashirika binafsi pamoja na washiriki kutoka wizara mbalimbali.Picha na Gadiola Emmanuel
  Washiriki wa  mkutano wa 7 wa jumuiko la maliasili  uliofanyika jijini Arusha na kuhudhuriwa na mashirika binafsi pamoja na washiriki kutoka wizara mbalimbali.Picha na Gadiola Emmanuel
  Viongozi mbalimbali wa jumuiko la maliasili wakiwa katika mkutano wa 7 wa jumuiko hilo uliofanyika jijini Arusha na kuhudhuriwa na mashirika binafsi pamoja na washiriki kutoka wizara mbalimbali.Picha na Gadiola Emmanuel
 Washiriki wa  mkutano wa 7 wa jumuiko la maliasili  uliofanyika jijini Arusha wakiwa katika picha ya pamoja, ,mkutano huo ulihudhuriwa na mashirika binafsi pamoja na washiriki kutoka wizara mbalimbali.Picha na Gadiola Emmanuel
Washiriki wa  mkutano wa 7 wa jumuiko la maliasili  uliofanyika jijini Arusha na kuhudhuriwa na mashirika binafsi pamoja na washiriki kutoka wizara mbalimbali .Picha na Gadiola Emmanuel 
Washiriki wa  mkutano wa 7 wa jumuiko la maliasili  uliofanyika jijini Arusha na kuhudhuriwa na mashirika binafsi pamoja na washiriki kutoka wizara mbalimbali.Picha na Gadiola Emmanuel 
Mwakilishi wa Shirika la WWF ,Sware Semesi  akizungumza katika  mkutano wa 7 wa jumuiko la maliasili  uliofanyika jijini Arusha na kuhudhuriwa na mashirika binafsi pamoja na washiriki kutoka wizara mbalimbali.Picha na Gadiola Emmanuel 
Picha ya baadhi ya wafanyakazi wa Jumuiko la Maliasili Tanzania waliokuwepo Kwenye mkutano wa 7 wa jumuiko la maliasili  uliofanyika jijini Arusha na kuhudhuriwa na mashirika binafsi pamoja na washiriki kutoka wizara mbalimbali.Picha na Gadiola Emmanuel
Wasemaji Wakuu wa   mkutano wa 7 wa jumuiko la maliasili  uliofanyika jijini Arusha na kuhudhuriwa na mashirika binafsi pamoja na washiriki kutoka wizara mbalimbali.Picha na Gadiola Emmanuel 

Na Ferdinand Shayo wa Wazalendo 25 Blog ,Arusha.



Mwenyekiti wa Bodi wa Jumuiko la Maliasili nchini Dr.Suma Kaare amemtaka Raisi John Pombe Magufuli adhibiti upotevu wa mali asili za wanyama pori na misitu uliokithiri katika maeneo mengi nchini ili kunusuru uhai wa maliasili.



Suma Kaare amesema  hayo katika mkutano wa 7 wa jumuiko la maliasili  unaoendelea jijini Arusha,Kaare amesema kuwa jukwaa hilo litashirikiana na Rais huyo katika  kuhakikisha kuwa maliasili zinalindwa na kuwanufaisha Watanzania kwa kiwango stahiki.



“Tunajua Rais wetu mpya ana kazi  kubwa  ya kulinda maliasili za nchi hii kama ilivyo kauli mbiu yake ya “kazi tu” tunaamini atazuia upotevu mkubwa wa rasilimali unaofanywa na watendaji wasio waaminifu” Alisema Kaare



Mratibu wa Masuala ya misitu katika shirika la uhifadhi wa maliasili na Mazingira (wwf) ,Isaac Malungu amesema kuwa asilimia 90% ya nishati inayotumika nchini inatokana na kuni pamoja na mkaa hali ambayo inaathiri misitu na kutishia uhai wa maliasili nchini hivyo ameitaka serikali ihimize matumizi ya nishati mbadala ili kunusuru mazingira yanaoharibiwa kila kukicha.



Malungu alisema kuwa kilimo cha kuhama hama pamoja na ukataji miti ovyo umekua ukisababisha uharibifu wa mazingira na hata kupelekea hecta laki 4 za misitu kupotea kila mwaka kutokana na shughuli hizo.



Mkurugenzi wa  Shirika la AWF,John Salehe Alisema kuwa mabadiliko ya tabia ya nchi yamesababisha hali ya ukame inayowaathiri wanyama pamoja na mimea hivyo kuathiri uhifadhi kwa ujumla .



Salehe alisema kuwa juhudi zaidi zinapaswa kuchukuliwa ikiwemo upandaji wa miti pamoja na kutunza misitu ili kurejesha uoto wa asili uliopotea.

No comments:

Post a Comment