Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan,
akisaini kwenye Kitabu cha maombolezo ya msiba wa Mjukuu wa Mhe. Rais
Dkt. John Magufuli, Maryfaustna Mlyambina, aliyefariki Nov 11, 2015.
Shughuli za kuagwa mwili wa marehemu zilifanyika Nov 13, 2015 Kimara
jijini Dar es Salaam, na baadaye msiba huo kusafirishwa kuelekea Mkoani
Mwanza kwa maziko.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan,
akitoa heshima za mwisho mbele ya jeneza lenye mwili wa Mjukuu wa Mhe
Rais John Magufuli, marehemu Maryfaustna Mlyambina, wakati wa shughuli
za kuaga zilizofanyika Kimara jijini Dar es Dalaam, Nov 13, 2015.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan,
akimfariji Mhe. Rais Dkt. John Magufuli, wakati wa shughuli za kuaga
mwili wa marehemu Maryfaustna Mlyambina zilizofanyika Kimara jijini Dar
es Dalaam. Marehemu ni mjukuu wa Mhe Rais.
Wazazi wa marehemu wakiwa na baadhi ya wanafamilia, wakati wa shughuli za kuaga mwili wa marehemu.
Rais
Dkt. John Magufuli (wa tatu kuli) Makamu wake (wa Nne kulia) Rais
Mstaafu Jakaya Kikwete, Mke wa Rais,Mama Janeth Magufuli (kulia) na Mke
wa Rais Mstaafu, Mama Salma Kikwete (kushoto) wakishiriki ibada maalum
ya kumuombea marehemu wakati wa shughuli za kuaga mwili zilizofanyika
Kimara jijini Dar es Salaam, Nov 13, 2015.
Sehemu ya wanafamilia ya wafiwa katika ibada hiyo.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli, akitoa heshima
za mwisho mbele ya jeneza lenye mwili wa Mjukuu wa Mhe Rais John
Magufuli, marehemu Maryfaustna Mlyambina, wakati wa shughuli za kuaga
zilizofanyika Kimara jijini Dar es Dalaam,Nov 13, 2015.
Mke wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Janeth Magufuli, akitoa
heshima za mwisho mbele ya jeneza lenye mwili wa Mjukuu wa Mhe Rais,
marehemu Maryfaustna Mlyambina, wakati wa shughuli za kuaga
zilizofanyika Kimara jijini Dar es Dalaam, Nov 13, 2015.
Rais
Mstaafu wa awamu ya Nne, Dkt. Jakaya Kikwete, akitoa heshima za mwisho
mbele ya jeneza lenye mwili wa Mjukuu wa Mhe Rais John Magufuli,
marehemu Maryfaustna Mlyambina, wakati wa shughuli za kuaga
zilizofanyika Kimara jijini Dar es Dalaam,leo Nov 13, 2015.
Baadhi
ya kinamama wakibeba Jeneza lenye mwili wa marehemu Mjukuu wa Rais Dkt.
John Magufuli, baada ya shughuli za kuaga mwili zilizofanyika Kimara, jijini Dar es Salaam.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan,
akiagana na Mama mzazi wa marehemu na baadhi ya wanafamilia wafiwa
Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, wakati aliposindikiza
msiba wa mjukuu wa Mhe. Rais, marehemu Maryfaustna Mlyambina, Nov
13, 2015.
Picha na OMR
No comments:
Post a Comment