Msajili
wa Vyama vya Siasa Jaji Francis Mutungi akizungumza na waandishi wa
habari hawapo pichani juu ya utofauti wa itikadi wa vyama ndiyo
ukomavu wa demokrasia nchini hivyo ni jambo la busara kuvumiliana na
kufanya siasa za kistaarabu, ameyasema hayo wakati wa kikao hicho
kimefanyika leo jijini Dar es Salaam kulia ni Balozi wa Amani Mrisho
Mpoto na kushoto ni Balozi wa Amani Christina Shusho.
Balozi wa Amani Mrisho Mpoto akifafanua jambo katika kikao hicho leo jijini Dar es Salaam.
Msajili wa Vyama vya Siasa Jaji Francis Mutungi, katika kikao kilicho fanyika leo jijini Dar es Salaam.
(Picha na Emmanuel Massaka)
Na Magreth Kinabo-maelezo
OFISIya
Msajili wa Vyama Vya Siasa imewaasa na kuwataka viongozi wote
wa vyama vya siasa kutoa kauli na maelekezo kwa wafuasi wao na
wanachama wa vyama vyao kutoshiriki katika aina yoyote ile ya uvunjifu
wa amani hususan katika kipindi cha kuelekea Uchaguzi Mkuu na baada ya
uchaguzi huo.
Hayo
yamesemwa leo na Msajili wa Vyama Vya Siasa, Jaji Francis Mutungi
wakati akizungumza na waandishi wa habari leo kwenye ukumbi wa mikutano
uliopo katika ofisi hiyo jijini Dares Salaam.
“Dhamana ya
nchi iko mikononi mwenu,ushawishi wenu kuhusu amani katika kipindi hiki
ndio utakaoliokoa taifa la Tanzania ama utaliingiza taifa katika
vurugu na mfarakano,” alisema Jaji Mutungi.
Jaji
Mutungi alisema katika kipindi cha kampeni kumekuwepo na viashiria vya
uvunjifu wa amani miongoni mwa jamii yakiwemo baadhi ya makundi ya
wanachama, wafuasi na mashabiki wa vyama siasa.
“Makundi
hayo yanadiriki kutoa maneno ya kejeli, matusi, kuvamia, kupigana, hata
kujeruhi makundi mengine, ambayo siyo ya upande wao. Hali iiachwe mara
moja ili kuiweka nchi yetu Tanzania katika hali ya amani na kuiepusha
kuingia kwenye vurugu, mfarakano na machafuko yasiyokuwa na ulazima.
“Dumisheni
amani na kamwe tusijiingize kwenye siasa zinazoleta mfarakano na
uvunjifu wa amani, kumbukeni kuna maisha baada ya uchaguzi na amani ya
nchi yetu ni fahari yetu sote,alisema Mutungi.
Aliongeza
ni vyema Watanzania, wakatambua kwamba utofauti wa itikadiya vyama ndio
ukomavu wa demokrasia nchini hivyo ni jambo la busara kuvumiliana na
kufanya siasa za kiustaarabu.Hivyo kutovumiliana kwa utofauti wetu wa
itikadi za kisiasa kunaweza kulata madhara makubwa kwa jamii
itakatopelekea idadi kubwa ya Watanzania kupata athari ikiwemo ulemavu,
vifo, ukimbizi,njaa na maradhi.
Aidha
ofisi hiyo imetoa rai kwa waandishi wa habari watumie kalamu zao vysema
kuhubiri amani na kuepuka kuandika habari za uchochezi, bali
wawasaidie wananchi kupata taarifa sahihi zitakazowasaidia kufanya
maamuzi wakati wa kuchagua viongozi wao.
Kwa
upande wao mabalozi wa amani, ambao ni Mrisho Mpoto na Christina Shusho
walisema kwa nyakati tofauti kuwa wamejitolea kuhubiri amani kupitia
fani yao ili nchi yetu iendelee kuwa na amani.
Akizungumzia
suala hilo, Mpoto aliwapa changamoto waandishi wa habari wajiulize kuwa
wana mchango gani katika nchi yao ili kuhakikisha inakuwa na amani.
Hivyo wanapoandika habari yoyote wakumbuke kwamba kuna watoto, yatima,
walemavu na wajane, isije ikawa ni chanzo cha kuvuruga amani.
Naye Shusho alisema kwamba yeye si mfuasi wa chama chochote,bali balozi wa kuhubiri amani.
Ofisi
hiyo imetoa kauli hiyo, kwa kuwa ndiyo yenye jukumu la kuhakikisha
ukuaji wa demokrasia unakuwepo kulingana na sheria, kanuni na taratibu
zilizowekwa kikatiba.
No comments:
Post a Comment