|
Mwanafunzi
Fuad Thabit kutoka Feza Boys Secondary aliyeibuka mshindi wa kwanza
shule za sekondari katika Shindano la Genius-Cup akipokea cheti na
zawadi yake ya shilingi 300,000 toka kwa mgeni rasmi wa hafla hiyo,
Ofisa Mkuu wa Utafiti taasisi ya COSTECH, Athman Mgumia. |
|
Wanafunzi
Sita Washindi wa Shindano la Genius-Cup (mbele) wakiwa katika picha ya
pamoja na vyeti vyao mara baada ya kuibuka washindi. Nyuma yao ni meza
kuu katika hafla ya kuwazawadia ikipata picha ya ukumbusho na mabingwa
hao. |
|
Mkurugenzi wa Shule za Fedha Tanzania akizungumza katika hafla ya kuwazawadia washindi wa shindano la Genius-Cup. |
|
Baadhi
ya wanafunzi walioingia fainali katika shindano la kuwatafuta washindi
wa shindano la Genius-Cup wakifuatilia hafla hiyo jana. |
|
Ofisa
Mkuu wa Idara ya Elimu kutoka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi,
Fredrick Shuma akizungumza katika hafla ya shindano la Genius-Cup jana. |
|
Baadhi ya walimu na wazazi waliowaleta washiriki na kufanikisha ushindi wao wakiwa katika hafla hiyo jana. |
|
Mgeni
rasmi katika hafla ya kuwazawadia washindi wa Shindano
la Genius-Cup mgeni rasmi wa hafla hiyo, Ofisa Mkuu wa Utafiti taasisi
ya COSTECH, Athman Mgumia (wa pili kulia) akiwa na viongozi wengine wa
meaza kuu. Wa kwanza kulia ni Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Wavulana ya
Feza, Ibrahim Yunus. |
|
Burudani toka kwa wanafunzi ikiendelea...! |
|
Mmoja wa wanafunzi washindi wa shindano la Genius-Cup (kushoto) akipongezwa mara baada ya kupokea cheti na zawadi yake. |
|
Mwanafunzi
Shammah Kiunsi (kushoto) wa shule za msingi Mkoa wa Mbeya aliyeibuka
msindi wa pili na kujishindia kitita cha shilingi 200,000 akipokea cheti
na zawadi yake toka kwa mgeni rasmi katika hafla ya shindano
la Genius-Cup jana. |
|
Mmoja
wa washindi katika shindano la Genius-Cup, Fuad Thabit (katikati)
ambaye ni mshindi wa kwanza kutoka Feza Boys Secondary akipiga picha na
viongozi wa meza kuu katika hafla hiyo jana. |
WANAFUNZI
Sita walioibuka mabingwa wa Shindano la Genius-Cup la masomo ya sayansi
na hisabati wamezawadiwa zawadi zao jana katika fainali za mashindano
hayo zilizofanyika katika Shule ya Wavulana ya Feza Sekondari iliyopo
Tegeta Jijini Dar es Salaam.
Shindano
hilo lililoshindanisha shule mbalimbali za msingi na sekondari nchini
Tanzania na kuratibiwa na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kwa
kushirikiana na uongozi wa Shule za Feza nchini limejumuisha zaidi ya
wanafunzi 1,486 limelenga kukuza vipaji vya wanafunzi hasa masomo ya
sayansi na hisabati.
Akizungumza
na mwandishi wa habari hizi mara baada ya kumalizika kwa shindano hili,
Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Wavulana ya Feza, Ibrahim Yunus alisema
wanafunzi sita walioibuka washindi na kupatia vitita vya fedha ni pamoja
na Fuad Thabit mshindi wa kwanza kutoka Feza Boys Secondary
aliyejipatia shilingi 300,000 na Zulfa Khamis msindi wa pili toka shule
za sekondari Mkoani Tanga aliyejishindia shilingi 200,000.
Bw.
Yunus alimtaja mshindi mwingine wa kwanza shule za msingi ni Mvano
Michael Cabangoh kutoka shule ya Green Acres aliyejishindia shilingi
300,000 na Shammah Kiunsi mwanafunzi wa shule ya msingi kutoka Mkoa wa
Mbeya aliyejishindia kitita cha shilingi 200,000 pamoja na Dorice Ernest
Msafiri mshindi wa tatu (msingi) kutoka Mkoa wa Dodoma Ignatius School
aliyejinyakulia shilingi 150,000/-.
Akifafanua
zaidi Mwalimu Mkuu wa Sekondari ya Wavulana ya Feza, Bw. Yunus alisema
wanafunzi walioingia fainali na kukutanishwa kwa pamoja ni 70 kati ya
wanafunzi 1,486 walioshiriki katika kinyang'anyiro hicho. Aliongeza kuwa
hii ni mara ya pili shindano la GENIUS CUP linafanyika kwani kwa mara
ya kwanza lilifanyika mwaka jana huku likilenga kukuza mapenzi ya masomo
ya sayansi na hisabati kwa wanafunzi wa Tanzania.
Kwa
upande wake Ofisa Mkuu wa Idara ya Elimu kutoka Wizara ya Elimu na
Mafunzo ya Ufundi, Fredrick Shuma akizungumza kabla ya kukabidhi vyeti
kwa wanafunzi washindi aliupongeza uongozi wa shule za fedha nchini kwa
kuliendeldeza shindano hilo kwani linachangia kuleta chachu ya mapenzi
kwa masomo ya sayansi na hisabati kwa wanafunzi nchini Tanzania ambao
wamekuwa wakiyaogopa masomo ya sayansi.
No comments:
Post a Comment