Mfanyaakzi
wa Airtel, (kulia), akijaza fomu ya kujiunga na mpango wa uchangiaji wa
hiari (Wote Scheme), wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, wakati wa ufunguzi wa
wiki ya Wafanyakazi wa Airtel, makao makuu ya kampuni hiyo ya simu za
mikononi, jijini Dar es Salaam, Septemba 26, 2015.
Wafanyakazi
wa Airtel, wakipatiwa maelezo juu ya huduma mbalimbali zitolewazo na
PPF, wkati wa wiki ya wafanyakazi wa kampuni hiyo ya simu makao makuu ya
Airtel, Morocco jijini Dar es Salaam, Septemba 26, 2015.
Meneja
Masoko wa PPF, Elihuruma Ngowi, (kulia), akizungumza jambo na Meneja
Uhusiano wa Airtel, Jackson Mbando, wakati wa ufunguzi wa wiki ya
Wafanyakazi wa Airtel
NA K-VIS MEDIA
MFUKO
wa Pensheni wa PPF, umevuna wanachama wapya kadhaa kwenye Wiki ya
Wafanyakazi wa kampuni ya simu za mikononi, Airtel, iliyoanza leo
Septemba 26, 2015 pale makao makuu ya Airtel, Morocco jijini Dar es
Salaam.
Akizungnumza
na waandishi wa habari wakati wa utoaji huduma kwa wafanyakazi hao,
Meneja Masoko wa PPF, Elihuruma Ngowi, amesema, Airtel ni moja ya
“Akaunti’ kubwa za PPF, kwa maana ya Mfuko kuwa na idadi kubwa ya
wanachama kutoka kampuni hiyo, hivyo wameitumia fursa hiyo kutoa elimu
ya huduma mbalimbali zitolewazo na Mfuko.
“Pamoja
na kusajili wanachama wapya chini ya Mpangop wa Wote Scheme, yaani
ucnangiaji wa hiari, pia tumewaeleza wanachama wetu kuhusu mafao mapya
yatolewayo na Mfuko kama fao la Uzazi.” Alifafanyua Ngowi.
Meneja
Msoko huo wa PPF pia alisema, Wanachama wa PPF kupitia mpango huo wa
wote scheme, wanaweza kujiunga na bima ya afya ya NHIF, ambapo PPF
inakuwa mdhamini wa wanachama wake kupitia mpango huo wa uchangiaji wa
hiari (Wote Scheme).
Afisa
Uwekezaji Mwandamizi wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Anna Shayo, (kulia),
akimsikiliza Mwanachama wa Mfuko huo, wakati wa utoaji huduma kwenye
wiki ya wafanyakazi wa kampuni ya simu za mikononi ya Airtel, makao
makuu ya kampuni hiyo jijini Dar es Salaam
Afisa
wa Operesheni wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Kanda ya Kinondoni jijini
Dar es Salaam, Saluna Aziz Ally, (kushoto), akimeuelekeza Mwanachama wa
Mfuko huo jinsi ya kupata taarifa za michango yake kupitia simu ya
mkunoni, huduma ijulikanayo kama “PPF Taarifa), wakati wa ufunghuzi wa
wiki ya wafanyakazi wa Airtel, iliyoanza leo Sptemba 26, 2015 pale makao
makuu ya kampuni hiyo ya simu za mikononi, Morocco jijini Dar es Salaam
Mwanachama
mpya wa PPF Sitti Mweneyuni, akijaza fomu za kujiunga na mpango wa
uchangiaji wa hiari (Wote Scheme), wakati wa ufunguzi wa wiki ya
wafanyakazi wa kampuni ya simu za mikononi, Airetel, jijini Dar es
Salaam
Mwanachama
mpya wa PPF akijaza fomu za kujiunga na mpango wa uchangiaji wa hiari
(Wote Scheme), wakati wa ufunguzi wa wiki ya wafanyakazi wa kampuni ya
simu za mikononi, Airetel, jijini Dar es Salaam
Afisa
Operesheni wa Kanda wa Mfuko wa Pensehni wa PPF, Upendo Singinika,
(kulia), akimpatia zawadi mwanachama wa Mfuko huo baadab ya kupatiwa
maelezo ya huduma mbaklimbali zitolewazo na Mfuko huo, kwenye ufunguzi
wa wiki ya wafanyakazi wa Airtel makao makuu ya kampuni hiyo ya simu za
mikononi jijini Dar es Salaam
Afisa Masoko wa PPF, Francis Kihinga, akimpatia maelezo ya kina mwanachama wa PPF
Abib
Kibiki, (kushoto), Afisa Masoko wa PPF, akimpatia maelezo Mfanyakazi
huyu wa Airtel, wakati wa wiki ya wafanyakazi wa Airtel
Afisa
operesheni wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Upendo Singinika, (kulia),
akishauriana jambo na Mtaalamu wa mifumo ya Computer wa Mfuko huo,
Gideon Mwashihongo, wakati wa wiki ya wafanyakazi wa Aiortel,ambapo PPF
ilitumia fursa hiyo kusajili wanachama wapya chini ya mpango wa Wote
Scheme
Mfanyaakzi
wa Airtel, (kulia), akitumia simu yake ya mkononi, kupata taarifa za
michango yake ya uanachama wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, kupitia huduma
ya PPF Taarifa
No comments:
Post a Comment