Na Chalila Kibuda.
WANAFUNZI waliosoma
Shule ya Forodhani na Sasa St.Joseph Cathedral wameanzisha
umoja wa shule hiyo kwa ajili ya kusaidia elimu pamoja na masuala ya
kijamii.
Wakizungumza nyakati tofauti wanafunzi waliosoma hapo
wamewataka wanafunzi kufuata nyayo zao kutokana na shule hiyo kuwa na historia
nzuri ambayo hadi sasa haijaweza kufutika.
Wamesema kuwa umoja huo utakuwa imara katika kusaidia
shule hiyo katika masuala mbalimbali ikiwemo na kusaidia jamii kutokana na
malezi walioyapata katika shule hiyo tangu Ukoloni.
Akizungumza
katika uzinduzi huo mwanafunzi aliosoma shule
hiyo,Miriamme Ziaror, amesema umoja wa wanafunzi waliosoma shule ya St
Joseph
convent school iliodumu kuanzia mwaka
1932 hadi 1969, na Forodhani Sekondari
ilokuwapo 1970 hadi 2008 ( ilitaifishwa na serikali) na baada ya hapo St
Joseph Cathedral High school 2009 (baada ya kurushwa kwa kanisa la
katoliki) hadi leo inatambulika St. Joseph & Forodhani ALUMNI .
Miriamme amesema katika shule hiyo kuna wanafunzi waliosoma shule hiyo, wanaoishi
nje ya nchi, wanaotoka Canada, Australia,
New Zealand Uingereza na Seychelles wameungana kuhudhuria mkutano huu wa
kishitoria wa kuanzisha umoja wa ALUMNI.
Amesema baadhi ya wanaWengine hawajafika Tanzania kwa
miaka zaidi ya 30. Wanarudi kuona shule
iliowalea.
Aidha amesema katika watu maarufu wanaotoka nchi za nje
atakuwapo Jaji Mkuu wa mahakama ya Rufaa Seychelles ambaye alisoma hapo na kumaliza kidato cha
nne mwaka 1968, na baada ya hapo, kuhamia Seychelles na wazazi wake alipo kuendelea na masomo ya juu.
Kwa upende wa Mbunge wa Viti Maalumu ,mwanafunzi wa shule
hiyo zamani Ashymaa Kwegyry ametaka wanafunzi kuwa wadhubutu na kuweza
kufanikisha ndoto zao.
Amesema amesoma shule kutokana na kuwa na ulemavu lakini
walimu walimfundisha na kuamini kuwa na anaweza kufanya kitu kama binadam
wengine.
Mwanafunzi
wa Zamani wa Forodhan,Miriamme Zailor akizungumza wakati wa uzinduzi wa
umoja wa wanafunzi waliosoma shule ambayo kwa sasa ni St.Joseph
Cathedral leo jijini Dar es Saalaam.
Mwananfunzi
wa zamani wa shule ya Sekondari ya St.Joseph hivi sasa, Ashymaa Kwegyry
akizungumza katika uzinduzi wa umoja wa wanafunzi waliosoma katika
shule hiyo jijini Dar es Salaam.
Wanafuzi walohitimu mwaka 2014 wakisoma lisala ya shule hiyo, Damian Mapalala na Nancy Kimario.
Baadhi
ya wanafunzi wanaosoma shule ya Sekondari ya St.Joseph walioshiriki
katika uzinduzi wa umoja wa wanafuzi waliosoma shule hiyo jijini Dar es
Salaam.
Baadhi
ya wanafunzi waliosoma shule ya Sekondari ya St.Joseph zamani wakiwa
wameshuriki katika uzinduzi wa wanafunzi waliosoma shule hiyo jijini Dar
es Salaam.
Wanafunzi wakitumbuiza katika uzinduzi huo jijini Dar es Salaam.
Wapigangoma wakipiga ngoma jijini Dar es Salaam katika uzinduzi huo.
Baadhi
ya wanafunzi wanaosoma shule hiyo wakiwa wamevalia mavazi ya kimasai
mara baada ya kucheza ngoma inayowakilisha kabila la wamasai katika
uzinduzi huo jijini Dar es Salaam leo.
Baadhi ya wanafunzi waliosoma shule hiyo zamani.
Picha ya pamoja ya baadhi ya wanafunzi waliosoma shule ya St.Joseph
Picha
ya pamoja ya wanakamati ya maandalizi ya uzinduzi wa Umoja wa wanafunzi
waliosoma shule ya St.Joseph mara baada ya kumalizika uzinduzi huo
jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wanafunzi waliosoma shule hiyo.
No comments:
Post a Comment