Makamu
Mkuu wa Chuo Kikuu Cha Dar Es Salaam, (Anayeshughulikia masuala ya
Utawala), Profesa David Mfinanga, (Watatu kushoto), akipeana mikono na
Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Abdul Njaidi,
(watatu kulia), wakati akipokea msaada wa magodoro 118 yaliyotolea wan
Mfuko huo kwenye hafla fupi iliyofanyika chuon I hapo, Agosti 24, 2015.
Magodoro hayo ni kwa ajili ya wanafunzi walioathiriwa na mogto uliozuka
kwenye bweni kitalu B kule hosteli za Mabibo, Aprili mwaka huu 2015.
NA K-VIS MEDIA
MFUKO
wa Pensheni wa PSPF, leo Agosti 24, 2015, umekipatia Chuo Kikuu Cha Dar
es Salaam, UDSM, magodoro 118 ili kusaidia huduma ya malazi kwa
wanachuo walioathirika kutokana na bweni lao kuungua moto kwenye hosteli
ya chuo hicho Mabibo jijini Dar es Salaam Aprili mwaka huu.
Akikabidhi
msaada huo kwa Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam,
(Anayeshughulikia masuala ya Utawala), Profesa David A. Mfinanga, Afisa
Uhusiano Mwandamizi wa PSPF, Abdul Njaidi, amesema, PSPF, iliguswa na
ajali hiyo ya moto ambayo iliyotokea kwenye bweni kitalu namba B na
kusababisha mamia ya wanachuo kupoteza mali zao.
“Kwa
kutambua kuwa wanachuo ni sehemu ya jamii ya Watanzania, na pia ni
wanachama watarajiwa wa Mfuko, tumeona tuchangia sehemu ya vifaa ili
wanafunzi waweze kurejean katika hali yao ya kawaida.” Alisema Njaidi.
Akitoa
shukrani zake, kwa niaba ya Chuo, Profesa Mfinanga aliishukuru PSPF,
kwa msaada huo ambao kwa hakika umesaidia pakubwa, kwani magodoro hayo
yatapelekwa kwa walengwa na hivyo kusaidia kuwapunguzia machungu
waliyoyapata kutokana na kuunguliwa vifaa vyao.
Kwa mujibu wa viongozi wa Chuo hicho, jingo hilo lilikuwa ,linakaliwa na wanachuo 788, wakati linawaka moto.
Profesa mfinanga (wapili kushoto), akitoa shukrani kwa niaba ya chuo mbele ya maafisa wa PSPF, viongozi wa wanachuo na wafanyakazi wa chuo hicho wakati wa hafla hiyo.
Afisa
Uhusiano wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Abdul Njaidi, (kushoto),
akizungumza na baadhi ya wafanyakazi wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam,
baada ya kukabidhi msaada huo, Agosti 24, 2015.
Paulina
Mabuga, mfanyakazi wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaa, (wapili kulia),
akizungumza kwenye hafla hiyo. Wakwanza kushoto ni Rais wa Serikali ya
Wanafunzi, Denis Bashulula
Profesa Mfinanga na Njaidi wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa serikali ya wanafunzi UDSM.
Mfanyakazi wa UDSM, akipita jirani na magodoro hayo.
No comments:
Post a Comment