Mgombea mwenza wa CCM nafasi ya urais, Bi. Samia Suluhu akiwasikiliza
akinamama wakimuelezea kero ya maji baada ya kumsimamisha na kumpa kero
hizo Jimboni Longido.
Wakinamama wilayani Longido wakiendelea kuteka maji kwa zamu baada ya
kumaliza kumueleza kero zao Bi. Samia Suluhu aliepita maeneo hayo.
Baadhi ya wanaCCM na wananchi wa Jimbo la Monduli wakiwa kwenye mkutano
wa hadhara wa mgombea mwenza nafasi ya urais wa CCM, Bi. Samia Suluhu.
Baadhi ya wanaCCM na wananchi wa Jimbo la Monduli wakiwa kwenye mkutano
wa hadhara wa mgombea mwenza nafasi ya urais wa CCM, Bi. Samia Suluhu.
Baadhi ya wanaCCM na wananchi wa Jimbo la Monduli wakiwa kwenye mkutano
wa hadhara wa mgombea mwenza nafasi ya urais wa CCM, Bi. Samia Suluhu. Mgombea mwenza wa CCM nafasi ya urais, Bi. Samia Suluhu akiwa katika vazi la kimasai alilopewa kama zawadi na wanaMonduli. Baadhi ya wajumbe wa kamati ya kampeni ya CCM taifa wakiwa katika mkutano wa hadhara wa mgombea mwenza Bi. Suluhu.
Baadhi ya wanaCCM na wananchi wa Jimbo la Monduli wakiwa kwenye mkutano
wa hadhara wa mgombea mwenza nafasi ya urais wa CCM, Bi. Samia Suluhu.
Bi. Samia Suluhu akimnadi mgombea ujumbe wa Jimbo la Monduli, Bi. Namelok Sokoine (kushoto) kwenye mkutano wa hadhara. Baadhi ya wanaCCM na wananchi wa Jimbo la Monduli wakiwa kwenye mkutano wa hadhara wa mgombea mwenza nafasi ya urais wa CCM, Bi. Samia Suluhu.
Bi. Samia Suluhu akimnadi mgombea ujumbe wa Jimbo la Monduli, Bi. Namelok Sokoine (kushoto) kwenye mkutano wa hadhara. Baadhi ya wanaCCM na wananchi wa Jimbo la Monduli wakiwa kwenye mkutano wa hadhara wa mgombea mwenza nafasi ya urais wa CCM, Bi. Samia Suluhu.
Na Joachim Mushi, Longido
WANAWAKE wa Wilayani Longido wamemsimamisha mgombea Mwenza wa urais
Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bi. Samia Suluhu njiani akielekea jukaani
kuhutubia wananchi wakimlilia kuwatatulia kero ya maji katika Kata ya
Longido ambapo kila familia imekuwa ikipata huduma hiyo mara moja kwa
wiki hali ambayo wamesema haikidhi mahitaji.
Bi.
Samia alilazimika kusimama eneo ambalo wanawake walikuwa wamefurika
wakichota maji kwa zamu huku kila familia ikipewa idadi ya ndoo kumi
mara moja kwa kila wiki kiwango ambacho akinamama wengi walisema
akikidhi mahitaji kwa familia zao.
Mgombea
huyo wa CCM aliwahakikishia akinamama hao kuwa yeye kama mwanamke
anajua shida ya maji inavyowatesa akinamama katika familia ikiwa huduma
hiyo inapokuwa tatizo katika upatikanaji wake, hivyo atalisimamia suala
hilo.
Alisema
Serikali ya CCM itakapoingia madarakani imetenga shilingi bilioni 13
kwa ajili ya kupeleka maji eneo la Longido mradi ambao utamaliza kero ya
maji eneo hilo.
Akizungumza
katika mkutano wa hadhara Longido Bi. Suluhu alisema kwa kuwawezesha
wafugaji wa eneo hilo wamepanga kujenga mabwawa ya kuvuna na kuhifadhi
maji kwa ajili ya matumizi ya nyakati za ukame kwa baadhi ya maeneo,
ikiwa ni pamoja na kujenga majosho ya mifugo na kuwezesha madawa ya
mifugo kwa wafugaji ili kuwaendeleza.
"...Kazi
hii tutaifanya ndani ya kipindi kifupi mara tu baada ya kufanikiwa
kurudi madarakani, Serikali inayomaliza muda wake imefanya mengi na sisi
tutaendeleza na kuboresha zaidi. Alisema wanajua kilio cha mahakama
katika wilaya ya Longido hivyo mara baada ya kuingia madarakani
wataijenga.
Alisema
akiwa njiani katika mikutano ya kampeni zake ameshuhudia uwepo wa ukame
katika vijiji lakini anawahakikishia hakuna mwananchi ambaye atakufa na
njaa endapo hali hiyo ya ukame itaendelea, kwani serikali ya CCM katika
ghala la chakula ina akiba ya kutosha.
Mgombea
huyo mwenza wa CCM pia alifanya mkutano wa hadhara katika Jimbo Monduli
aliwaomba wanaMonduli kumpigia kura ya ndio mgombea urais kwa tiketi ya
CCM, Dk. John Pombe Magufuli ili aweze kutekeleza ilani ya chama hicho
ambayo pia imejumuisha ujenzi wa barabara ya Sanya Juu hadi Longido na
Longido hadi Mto wa Mbu wilayani Longido.
Aliwaomba
wanaMonduli kumchagua mgombea ubungw wa Jimbo la Monduli kwa tiketi ya
CCM, Bi. Namelok Sokoine kwani mgombea huyo anarekodi na historia nzuri
ya utendaji kama alivyokuwa babayake marehemu, Edward Moringe Sokoine.
Aliwaomba pia kuwachagua madiwani wa CCM ili waweze kufanya kazi kwa
ushirikiano kama timu.
No comments:
Post a Comment