Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akiweka saini hati ya Muswada wa Sheria ya Mafuta
na Gesiasilia Jumanne, Agosti 4, 2015 katika Ukumbi mpya wa Ikulu, Dar
Es Salaam akishuhudiwa na Waziri wa Nishati na Madini Mhe George
Simbachawene na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Mhandisi Ngosi Mwihava.
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akiweka saini hati ya Muswada wa Usimamizi wa
Mapato ya Mafuta na Gesiasilia Jumanne, Agosti 4, 2015 katika Ukumbi
mpya wa Ikulu, Dar Es Salaam akishuhudiwa na Waziri wa Nishati na Madini
Mhe George Simbachawene na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Mhandisi Ngosi
Mwihava.
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akigonga muhuri wake hati ya Muswada wa Sheria ya
Mafuta na Gesiasilia Jumanne, Agosti 4, 2015 katika Ukumbi mpya wa
Ikulu, Dar Es Salaam akishuhudiwa na Waziri wa Nishati na Madini Mhe
George Simbachawene na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Mhandisi Ngosi
Mwihava.
Rais
Kikwete akipeana mikono na Waziri wa Nishati na Madini Mhe George
Simbachawene baada ya kuweka saini kuridhia Muswada wa Sheria ya Mafuta
na Gesiasilia Jumanne, Agosti 4, 2015 katika Ukumbi mpya wa Ikulu, Dar
Es Salaam.
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akiweka saini kuridhia Muswada wa Usimamizi wa
Mapato ya Mafuta na Gesiasilia Jumanne, Agosti 4, 2015 katika Ukumbi
mpya wa Ikulu, Dar Es Salaam akishuhudiwa na Waziri wa Fedha Mhe. Saada
Mkuya na Katibu Mkuu wizara hiyo Dkt. Servacius Likwelile.
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akipeana mikono na Waziri wa Fedha Mhe. Saada
Mkuya baada ya kuweka saini kuridhia Muswada wa Usimamizi wa Mapato ya
Mafuta na Gesiasilia Jumanne, Agosti 4, 2015 katika Ukumbi mpya wa
Ikulu, Dar Es Salaam.
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akiweka saini kuridhia Muswada wa Tume ya Walimu
Jumanne, Agosti 4, 2015 katika Ukumbi mpya wa Ikulu, Dar Es Salaam
akishuhudiwa na Dkt. Shukuru Kawambwa ambaye ni Waziri wa Elimu na
Mafunzo ya Ufundi na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Profesa Sifuni Mchome.
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akipeana mikono na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya
Ufundi Dkt. Shukuru Kawambwa baada ya kuweka saini kuridhia Muswada wa
Tume ya Walimu Jumanne, Agosti 4, 2015 katika Ukumbi mpya wa Ikulu, Dar
Es Salaam kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Profesa Sifuni Mchome.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipeana mikono na Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Profesa Sifuni Mchome
baada ya kuweka saini kuridhia Muswada wa Tume ya Walimu Jumanne, Agosti 4, 2015 katika Ukumbi mpya wa Ikulu, Dar Es Salaam.
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete, Makamu wa Rais Dkt. Mohamed Gharib Bilali, Katibu
Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue katika picha ya pamoja na Mheshimiwa
George Simbachawene, Waziri wa Nishati na Madini, Mheshimiwa Saada
Mkuya, Waziri wa Fedha na Mhe. Dkt. Shukuru Kawambwa, Waziri wa Elimu
na Mafunzo ya Ufundi baada ya hafla ya kuweka saini na kuridhia miswada
ya Sheria ya Mafuta na Gesiasilia, Muswada wa Uwazi na Uwajibikaji,
Muswada wa Usimamizi wa Mapato ya Mafuta na Gesiasilia, Muswada wa
Masoko ya Bidhaa na Muswada wa Tume ya Walimu.
PICHA NA IKULU
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete
leo, Jumanne, Agosti 4, 2015, ametia saini Miswada ya Sheria mitano
hadharani ikiwa ni hatua yake ya mwisho kabisa kuridhia Miswada ya
Sheria akiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Katika
sherehe iliyofanyika katika Ukumbi mpya wa Ikulu, Dar Es Salaam,Rais
Kikwete ameridhia Muswada wa Sheria ya Mafuta na Gesiasilia, Muswada wa
Uwazi na Uwajibikaji, Muswada wa Usimamizi wa Mapato ya Mafuta na
Gesiasilia, Muswada wa Masoko ya Bidhaa na Muswada wa Tume ya Walimu.
Katika
sherehe hizo zilizohudhuriwa na mamia ya wageni waalikwa, mawaziri
wanaohusika na sekta hizo, Mheshimiwa George Simbachawene ambaye ni
Waziri wa Nishati na Madini, Mheshimiwa Saada Mkuya ambaye ni Waziri wa
Fedha na Mhe. Dkt. Shukuru Kawambwa ambaye ni Waziri wa Elimu na Mafunzo
ya Ufundi wametoa maelezo ya miswada hiyo mitano kabla haijaridhiwa na
Rais Kikwete.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Mohamed
Gharib Bilal na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue pia
wamehudhuria sherehe hizo ambazo vile vile zimehudhuriwa na mawaziri wa
Serikali, mabalozi, wawakilishi wa taasisi zisizokuwa za Kiserikali
(NGO’s) na wadau wengine wa sekta ambazo Miswada yake imeridhiwa.
Hiyo
ni mara ya pili kwa Rais Kikwete kuridhia Miswada ya Sheria hadharani.
Mara ya kwanza ilikuwa mwaka 2009 wakati Rais Kikwete aliporidhia
hadharani Muswada wa Sheria ya Matumizi ya Fedha katika Uchaguzi.
Aidha,
hiio ni mara ya mwisho kwa Rais Kikwete kuridhia Miswada ya Sheria
nchini kabla ya kuondoka madarakani mwanzoni mwa Novemba, 2015. Rais
tayari amelivunja Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
4 Agosti, 2015
No comments:
Post a Comment