Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Ally Rufunga (kulia) akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika lisilo la Kiserikali la Ariel Glaser Pediatric AIDS Healthcare Initiative (AGPAHI), Laurean Bwanakunu aliyekwenda kumuaaga ofisini kwake baada ya Rais Jakaya Kikwete kumteua kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD). (Picha na Francis Dande)
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Ally Rufunga (katikati) akizungumza na uongozi wa Shirika lisilo la Kiserikali la AGPAHI uliokwenda ofisini kwake wakati Mkurugenzi Mkuu wa shirika hilo alipokwenda kumuaga.
Meneja Miradi wa Shirika la AGPAHI kwa Mikoa ya Shinyanga & Simiyu, Dk. Gastor Njau (kushoto) akifafanua jambo.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la AGPAHI anayemaliza muda wake, Laurean Bwanakunu akifafanua jambo.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga akisisitiza jambo....
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga.
Mkurugenzi Mkuu wa AGPAHI akimsikiliza kwa makini Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Ally Rufunga.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Ally Rufunga akifafanua jambo wakati uongozi wa Shirika la AGPAHI ulipomtembelea ofisini kwake.
Mkurugenzi Mkuu wa AGPAHI anayemaliza muda wake.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la AGPAHI, Laurean
Bwanakunu (kushoto) akimkabidhi cheti cha shukrani Mkuu wa Mkoa wa
Shinyanga, Ally Rufunga, wakati alipokwenda kumuaga ofisini kwake baada
ya kuteuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD).
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Ally Rufunga akisoma cheti cha shukrani alichokabidhiwa na Mkurugenzi Mkuu wa shirika la AGPAHI anayemaliza muda wake.
Cheti cha shukurani alichokabidhiwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga.
Mkuu
wa Mkoa wa Shinyanga, Ally Rufunga (wa pili kulia) akiwa katika picha ya
pamoja na baadhi ya viongozi wa Shirika la AGPAHI. Wa pili kushoto ni
Mkurugenzi Mkuu wa shirika hilo anayemaliza muda wake, Meneja Miradi wa
Shirika hilo, Dk. Gastor Njau (wa kwanza kushoto) na Mratibu wa Programu
ya Mawasiliano na Huduma za Jamii, Jane Shuma (wa kwanza kulia).
Na Mwandishi Wetu, Shinyanga
Na Mwandishi Wetu, Shinyanga
MKUU
wa Mkoa wa Shinyanga, Ally Rufunga amesema kasi ya maambukizi ya Virusi
Vya Ukimwi mkoani hapa imepungua kutoka asilimia 9.1 mwaka 2011 hadi
asilimia 4.9 mwaka 2014.
Rufunga
alisema hayo ofisini kwake wakati akiagana na Mkurugenzi Mkuu wa Ariel
Glaser Pediatric Aids Healthcare Initiative (AGPAHI), Laurean Bwanakunu
ambaye ameteuliwa na Rais Jakaya Kikwete kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Bohari
ya Dawa (MSD) hivi karibuni.
Akizungumza
mbele ya waandishi wa habari, Rufunga hakusita kupongeza juhudi za
shirika hilo katika kuhakikisha linapambana na maambukizi mapya ya VVU
ili kufika kwenye ziro tatu.
“Wakati
mnaingia Shinyanga mwaka 2011 kasi yetu ilikua kubwa kuliko ile ya
kitaifa na hadi kufika Juni,2015 tulifika asilimia 4.1 japo hili
halijathibitishwa na Wizara ya Afya ila tumeshafika huko,” alisema mkuu
huyo wa mkoa.
Alisema
shirika la AGPAHI limejenga vituo bora vya kutolea huduma za tiba na
matunzo (CTCs) kwenye vituo vya afya na zahanati mbalimbali mkoani humo
na kuahidi kwamba ofisi yake itavitunza na kufanyia ukarabati pale
itakapohitajika.
“MSD
ndio uhai wetu hasa watanzania wanaoishi vijijini, nakutakia kazi njema…
waliokuteua hawakukosea, umefanya kazi nzuri kwa kushirikiana na
watumishi wengine wa AGPAHI".
“…Naamini
utaendelea kuwa kiongozi bora hata huko uendako, usiogope maneno maana
kazi za utumishi wa umma lazima maneno yawepo,” alisema Rufunga huku
akisisitiza kwamba wakazi wa Shinyanga wataendelea kushirikiana na
shirika hilo na kuenzi kazi wanazofanya.
Akimshukuru
kwa ushirikiano, Bwanakunu alisema kazi ya AGPAHI mkoani Shinyanga
ilikua rahisi kwa kuwa alipata ushirikiano kutoka kwa Mkuu huyo wa mkoa
na watumishi wengine wa idara ya afya.
“Naamini
ushirikiano nilioupata kwako utaendelea hata kwa atakayerithi nafasi
yangu. AGPAHI tulipoanza kazi, mkoa wa Shinyanga ulikua katika hali
mbaya ya maambukizi lakini sasa tunaamini tunaendelea kufanya kazi kubwa
ya kupunguza na ikibidi kuondoa kabisa maambukizi,” alisema Bwanakunu
kisha kumkabidhi cheti cha shukrani mkuu huyo wa mkoa.
No comments:
Post a Comment