Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akizindua Mpangokazi wa Kimataifa na Kanuni za Sheria ya kuzuia
usafirishaji haramu wa Binadamu, wakati wa hafla hiyo ya uzinduzi
iliyofanyika Agosti 21, 2015 kwenye Viwanja vya Karimjee, jijini Dar
es Salaam. Kulia ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mathias
Chikawe (kulia) ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kimataifa ya kupambana na
Usafirishaji Haramu wa Binadamu, Kinemo Kihonamo.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akimkabidhi Mpangokazi wa Kimataifa na Kanuni za Sheria ya kuzuia
usafirishaji haramu wa Binadamu, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe.
Mathias Chikawe, baada ya kuzindua rasmi Mpango kazi huo, kwenye Viwanja
vya Karimjee jijini Dar es Salaam, Agosti 21, 2015.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akizungumza wakati wa uzinduzi wa Mpangokazi wa Kimataifa na Kanuni za
Sheria ya kuzuia usafirishaji haramu wa Binadamu, uliyofanyika
Agosti 21, 2015 kwenye Viwanja vya Karimjee, jijini Dar es Salaam.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mathias Chikawe, akizungumza kabla ya
kumkaribisha mgeni rasmi kuzindua mpango kazi huo, wakati wa hafla ya
uzinduzi iliyofanyika Agosti 21, 2015 kwenye Viwanja vya Karimjee
jijini Dar es Salaam.
Baadhi
ya Wanafunzi waliohudhuria hafla ya uzinduzi huo wakimsikiliza mgeni
rasmi Makamu wa Rais, Dkt. Bilal, wakati akihutubia.
Baadhi
ya Wageni waalikwa waliohudhuria hafla ya uzinduzi huo wakimsikiliza
mgeni rasmi Makamu wa Rais, Dkt. Bilal, wakati akihutubia.
Baadhi ya Wanafunzi waliohudhuria hafla ya uzinduzi huo wakijisomea vipeperushi walivyogaiwa katika uzinduzi huo.
11
hadi 16:- Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, akiwa
katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi na wanafunzi waliohudhuria
hafla hiyo, baada ya uzinduzi.
Picha na OMR
No comments:
Post a Comment