Matukio : Binagi Media Group Yazindua kampeni yake ya "Piga Kura Epuka Kula" - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633

Thursday, 27 August 2015

Matukio : Binagi Media Group Yazindua kampeni yake ya "Piga Kura Epuka Kula"


Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Binagi Media Group George Marwa Binagi-GB Pazzo akionyesha Kitambulisho chake cha Kupigia Kura ikiwa ni katika Uzinduzi wa Kampeni yake ya KUHAMASISHA WATANZANIA WOTE kujitokeza Kupiga Kura 0ctoba 25 Mwaka huu kwa ajili ya Kuwachagua Viongozi watakaowatumikia. 
Kampeni hiyo inafahamika kwa jina la "MTANZANIA PIGA KURA, EPUKA KULA KWA AJILI YA MAENDELEO YAKO".

Katika Kampeni hiyo ambayo inaanza leo Agost 26, 2015 Wasomaji wa Mtandao huu pamoja na Wadau mbalimbali watapata fursa ya kutuma picha zao kwa ajili ya kuhamasisha zoezi zima la upigaji wa Kura pamoja na kuwa na uchaguzi wa Amani. Tuma picha yako kupitia Whatsupp namba +255 (0) 757 342 694 au Email binagimediagroup@gmail.com ukiambatanisha na ujumbe mfupi.

Huu ndio ujumbe wa GB Pazzo juu ya Kampeni hii ya Piga Kura, Epuka Kura "Kwangu mimi Piga Kura, Epuka Kula ina maana kwamba mimi ambae ni mpiga kura napaswa kuweka maslahi yangu binafsi pembeni na kupiga kura kwa ajili ya manufaa ya Watanzania wote maana nikiendekeza kula leo kuna uwezekano wa kushinda njaa kwa miaka mitano ijayo".
Binagi Media Group; Mtanzania Epuka Kula, Piga Kura Kwa Ajili Ya Maendeleo Yako"

No comments:

Post a Comment