BASATA yaipongeza Kamati ya Miss Universe Tanzania
Na Mwandishi wetu
Baraza
la Sanaa la Taifa (Basata) limeipongeza kampuni ya Compass
Communications Tanzania kwa kufanya mashindano bora ya Miss Universe
hapa nchini.
Kauli
hiyo imetolewa na Mratibu wa mashindano ya Miss Universe Fausta Magoti
wakati wa kufanya tathimini ya mashindano ya mwaka jana ambapo,
Caroline Benard aliibuka mshindi.
Magoti
alisema kuwa pamoja na kampuni ya Compass kuanza kushiriki katika
mashindano ya Miss Universe mwaka 2007, waliweza kufanya vyema na
kuitangaza Tanzania nje ya mipaka yake.
Mbali
ya kufanya vizuri katika mashindano ya kimataifa, Magoti alisema kuwa
wameridhishwa sana na utendaji wa kamati hiyo kwa kuteua majaji ambao
wamekuwa wakiwatangaza washindi ambao ni mfano bora kwa tabia kwa jamii.
“Washindi
wenu hawana kashfa katika jamii, mmeendesha mashindano yasiyokuwa na
malalamiko, kwa kwa kweli mnahitaji kupongezwa pamoja na kupata
changamoto nyingi kutoka kwa wadhamini,” alisema Magoti.
Alitoa
wito kwa waandaaji kupanua wigo wa mashindano yao na kuyafanya katika
mikoa mingi ili kujitangaza zaidi. “Najua changamoto kubwa ni kuapata
wadhamini, tunaomba mjitahidi ili kuyatangaza zaidi mashindano yenu,
Basata tumeridhishwa na utendaji wenu, tunataka mfanye bora zaidi ya
hapa,” alisema.
Mrembo
Flaviana Matata ambaye alimaliza katika hatua ya sita bora katika
fainali za mashindano ya mwaka 2007, kwa sasa amekuwa akifanya vyema nje
ya nchi katika sekta ya maonyesho ya mavazi au wanaminitindo.
“Ni
mashindano bora ambayo kwa kweli yametuvutia sana, tunaomba muongeze
bidii ili kuyaboresha zaidi kwani mashindano haya kwa sasa ni makubwa na
warembo wengi wanayaulizia jinsi ya kujiunga nayo,” alisema.
Mkurugenzi
wa Compass Communications ambaye pia ndiye mwandaaji mkuu wa mashindano
haya Maria Sarungi Tsehai aliishukuru Basata kwa usimamiaji bora wa
mashindano katika sekta ya sanaa nchini na kusema kuwa watajiathidi
kuongeza wigo wa washiriki kaika mashindano ya mwaka huu.
Maria alisema kuwa pamoja na changamoto zote wanazokabiliana nazo, bado wanahitaji msaada kutoka Basata ili kupata wadhamini.
“Basata
ni chombo cha serikali, mnaweza kutusaidia kupata wadhamini hata kwa
Wizara ya Maliasili na Utalii, sisi tunatangaza jina la nchi na utalii
pia, tunaamini kupitia kwenu, tunaweza kupata sapoti kubwa kutoka wizara
hiyo, Bodi ya Utalii (TTB) na mamlaka ya zake kama Tanapa.
No comments:
Post a Comment