Mtaalam
kutoka Kitengo cha Leseni, Wizara ya Nishati na Madini, Charles Gombe
akielezea hatua za Wizara katika kuboresha huduma za leseni za madini
kwa njia ya mtandao (Online Mining Cadastre Transactional Portal; OMCTP)
kwa wachimbaji wa madini (hawapo pichani) mjini Mtwara. Lengo la
mafunzo hayo lilikuwa ni kuwapa uelewa wachimbaji wa madini
kuhusu huduma hiyo pamoja na kuwasajili.
Baadhi
ya wachimbaji wadogo wakifuatilia kwa makini mada mbalimbali
zilizokuwa zinawasilishwa na wataalam kutoka Wizara ya Nishati na Madini
(hawapo pichani).
Kaimu
Kamishna Msaidizi wa Madini Kanda ya Kusini, Aidan Mhando akifungua
mafunzo kuhusu huduma za leseni za madini kwa njia ya mtandao
yaliyoshirikisha wachimbaji wa madini kutoka katika mkoa wa Mtwara.
Mwenyekiti
wa Chama cha Wachimbaji wa Madini kutoka Mkoa wa Mtwara (MTWAREMA),
Festo Balegele akifafanua jambo katika mafunzo hayo.
Kaimu
Kamishna Msaidizi wa Madini Kanda ya Kusini, Aidan Mhando ( wa pili
kutoka kushoto, waliokaa mbele) akiwa katika picha ya pamoja na
washiriki wa mafunzo hayo.
Mtaalam
kutoka Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) Mtwara, Juma Namuna akielezea
umuhimu wa wachimbaji wa madini kujiunga na mfuko huo ili kunufaika kwa
kupata mikopo.
Mtaalam
kutoka Kitengo cha Leseni, Wizara ya Nishati na Madini, Pendo Elisha
akielezea faida za kujiunga na huduma ya leseni za madini kwa njia ya
mtandao katika mafunzo hayo.
Mchimbaji mdogo wa madini ya chumvi, Hussen Abdalah akichangia mada kwenye mafunzo hayo.
Kaimu
Kamishna Msaidizi wa Madini Kanda ya Kusini, Aidan Mhando ( wa nne
kutoka kushoto, waliokaa mbele) akiwa katika picha ya pamoja na
wataalam wa Wizara ya Nishati na Madini na wachimbaji wa madini kutoka
Lindi walioshiriki mafunzo ya huduma ya leseni za madini kwa njia ya
mtandao yaliyofanyika mjini Lindi.
Mtaalam
kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Paul Mtulo akiweka mitambo sawa
kwenye gari la matangazo la Wizara kabla ya kuanza kwa kampeni ya
kuhamasisha wachimbaji wa madini kujiunga na huduma za leseni za madini
kwa njia ya mtandao mjini Lindi.
Na Greyson Mwase, Mtwara
Ofisi
ya Madini, Kanda ya Kusini yenye ofisi zake mjini Mtwara imeanza kutoa
huduma za leseni za utafutaji na uchimbaji wa madini ndani ya siku
moja tofauti na ilivyokuwa awali.
Hayo
yalisemwa na Kaimu Kamishna Msaidizi wa Madini Kanda ya Kusini, Aidan
Mhando katika mafunzo kuhusu huduma za leseni za madini kwa njia ya
mtandao (Online Mining Cadastre Transactional Portal; OMCTP)
yaliyoshirikisha wachimbaji wa madini mkoani Mtwara.
Mhando
alisema kuwa awali maombi yalikuwa yakichukua muda mrefu kutokana na
changamoto mbalimbali ikiwemo ya mtandao na kuongeza kuwa ofisi yake
imeboresha mtandao na kuanza kutoa leseni ndani ya siku moja.
Alisema
ofisi yake ina uwezo wa kushughulikia ombi moja la leseni ndani ya
nusu saa iwapo mwombaji atakuwa amekamilisha vigezo vyote
vinavyotakiwa.
Alieleza
kuwa tangu huduma ya mtandao iboreshwe ofisi ya madini imekuwa na uwezo
wa kushughulikia maombi 20 kwa siku tofauti na awali ambapo ilikuwa
inachukua muda mrefu.
Akielezea
mikakati ya ofisi yake katika utekelezaji wa mfumo mpya wa utoaji wa
huduma za leseni kwa njia ya mtandao, Mhando alisema ofisi imejipanga
kwa zoezi la kuhakikisha kuwa wateja wake wote wanaingizwa katika mfumo
huu na kunufaika na huduma hiyo.
Aliongeza
kuwa ili kuwafikia wachimbaji wa madini ya chumvi ambao idadi yako
kubwa ni wazee, ofisi yake imeweka utaratibu wa kuwatembelea kwenye
maeneo yao ya kazi, kuwapa elimu pamoja na kuwasajili kwenye mfumo
huu.
Akielezea
faida za mfumo mpya wa huduma za leseni za madini kwa njia ya mtandao
Mhando alisema kuwa mfumo utawawezesha wamiliki wa leseni za madini
kupata taarifa za leseni zao wakati wowote pamoja na kufanya malipo ya
leseni zao kwa njia ya mtandao yaani M-Pesa, Airtel Money na Tigo Pesa.
“Mfumo
huu utapunguza migogoro ambayo imekuwa ikijitokeza mara kwa mara kati
ya wachimbaji na kuondoa dhana ya kwamba kuna upendeleo kwenye utoaji
wa leseni za madini.” Alisema Mhando.
No comments:
Post a Comment