Mgombea ubunge wa Jimbo la Singida Kaskazini anayeomba kuchaguliwa tena, Lazaro Nyarandu akiwarudisha baadhi ya wananchi kurudi eneo la Mkutano wa kampeni na kuacha kushangaa helkopta. Mgombea ubunge wa Jimbo la Singida Kaskazini anayeomba kuchaguliwa tena, Lazaro Nyarandu akielekea eneo la mkutano pamoja na baadhi ya wananchi baada ya kutua na helkopta. Helkopta iliyomshusha gombea ubunge wa Jimbo la Singida Kaskazini anayeomba kuchaguliwa tena, Lazaro Nyarandu ikiwa inamsubiri. Mjumbe wa Kamati ya Kampeni Taifa, Mwigulu Nchemba (kushoto) wakimpongezana Katibu wa CCM Mkoa, Merry Mziku jimboni Iramba Magharibi. Bi. Suluhu kulia akizungumza neno na Mwigulu Nchemba na Bi. Mziku. Mjumbe wa Kamati ya Kampeni Taifa, Mwigulu Nchemba ambaye pia ni mgombea wa ubunge Jimbo la Iramba Magharibi akizungumza na wananchi kuinadi ilani ya CCM. Baadhi ya wanaCCM na wananchi wakiwa katika mkutano wa kampeni wa mgombea mwenza wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mjumbe wa Kamati ya Kampeni Taifa, Mwigulu Nchemba ambaye pia ni mgombea wa ubunge Jimbo la Iramba Magharibi akizungumza na wananchi kuinadi ilani ya CCM. Burudani kidogo kabla ya ilani kuendelea kunadiwa jimboni Iramba.
Na Joachim Mushi,
Singida
MGOMBEA ubunge wa Jimbo la Singida Kaskazini anayeomba kuchaguliwa tena,
Lazaro Nyarandu amenogesha kampeni za mgombea mwenza wa Chama Cha
Mapinduzi CCM, Bi. Samia Suluhu katika mikutano yake inayoendelea ya
kuinadi ilani ya CCM.
Nyarandu ambaye jana alishuka kwa helikopta ya kukodi Jimboni kwake
ikiwa ni muda mfupi baada ya mkutano wa kampeni kuanza alivuta hisia za
wanaCCM na wananchi katika mkutano huo.
Kama
hiyo haitoshi mgombea huyo wa ubunge alitumia helkopta hiyo kwenye
mikutano ya kampeni za mgombea mwenza ya Jimbo la Iramba Magharibi.
Akihutubia mkutano wa kampeni katika Kata ya Kengege, Jimbo la Iramba
Magharibi mkoani Singida, Bi. Suluhu aliwaomba wananchi kuipigia kura
CCM kwani ndani ya ilani yake imepanga kufanya mambo mazuri kwa
maendeleo ya mkoa huo. Alisema endapo watachanguliwa watajenga kiwanda
kikubwa cha kusafishia mafuta ya alizeti jambo ambalo litaongeza thamani
ya mazao kwa wakulima wa eneo hilo.
Aliongeza kuwa mbali na kiwanda hicho kikubwa kuwanufaisha wakulima pia
kitatoa nafasi za ajira kwa vijana ambapo jumla ya wafanyakazi 600
watapata ajira ndani ya kiwanda hicho, alisema baada ya Serikali ya
awamu ya nne kujenga shule za Sekondari za kata za kutosha na maabara
ilani mpya ya CCM imepanga kushughulikia suala la vifaa vya maabara hizo
ili ziweze kutumika kwa ufasaha.
Bi. Suluhu alisema Mkoani Singida imepanga kujenga hospitali kubwa ya
rufaa ambayo itakuwa ikitoa huduma katika mkoa huo na mikoa ya jirani,
pamoja na ujenzi wa barabara ya Ndago.
Aidha
akihutubia katika Mkutano mwingine Wilaya ya Ikungi aliahidi kufanya
jitihada za ujenzi wa hospitali ya Wilaya ya Ikungi ili kusongeza huduma
kubwa za afya kwa wanaIkungi, pamoja na kuvipatia umeme vijiji ambavyo
bado havijafikiwa na huduma hiyo kupitia mradi wa Wakala wa Umeme
Vijijini (REA) awamu ya pili.
Aliongeza kuwa licha ya maeneo ya mikoa ya singida kukabiliwa na tishio
la ukame aliwahakikishia hakuna raia atakayekufa njaa katika maeneo
hayo.
"...Serikali
imejipanga na ghala la kuhifadhi chakula lina akiba ya kutosha, hivyo
niwahakikishie hakuna mwanakijiji ambae atakufa kwa njaa.
Kwa
upande wake Mjumbe wa Kamati ya Kampeni Taifa, Mwigulu Nchemba ambaye
pia ni mgombea wa ubunge Jimbo la Iramba Magharibi akizungumza jimboni
hapo alisema ilani ya CCM imepanga kutekeleza miradi ya maji katika
Vijiji vya Mgundu, Kinampanda, Makunda pamoja na vijiji vingine
vinavyokabiliwa na kero ya maji.
Alisema
baadha ya mradi wa ujenzi wa shule za Sekondari za kata kufanikiwa
serikali itakayoundwa na CCM imepanga kusimamia ujenzi wa mabweni ili
kuwanusuru watoto wanaotembea umbali urefu kwenda shuleni pamoja huku
wasichana wakikabiliwa na changamoto za kubebeshwa mimba na kukatishwa
masomo yao.
Mwingulu aliwataka wananchi kutochagua vyama vingine kwani havina hoja
za msingi na vingine vinaazima hadi wagombea ili viweze kuwasimamisha.
Bi. Suluhu anaendelea na ziara yake ambapo sasa anaelekea Mkoa wa Dodoma
akiinadi ilani ya CCM.
No comments:
Post a Comment