Siasa Zetu :Mwanaharati wa Michezo Tanzania Mhe. Wilhem F.Gidabuday Ajitosa kwenye Ubunge wa Hanang kwa Tiketi ya CHADEMA - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633

Wednesday, 8 July 2015

demo-image

Siasa Zetu :Mwanaharati wa Michezo Tanzania Mhe. Wilhem F.Gidabuday Ajitosa kwenye Ubunge wa Hanang kwa Tiketi ya CHADEMA

A

Mwishoni mwa October 2015 (mwaka jana) nilisafiri hadi Butiama nyumbani kwa Mwl Nyerere.
Nilifika kwa maelekezo ya Madaraka Nyerere ambaye kwa mara ya kwanza nilikutana naye katika msafara wa kupanda mlima Kilimanjaro kuadhimisha miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania (2011).
Nilifurahi sana kulala nyumbani kwa baba wa taifa, nilijifunza mengi kuhusu yeye, kuhusu Tanzania na zaidi ya yote nilijifunza kupigania uhuru ambao si lazima uwe wa nchi tu, bali hata uhuru wa kujitambua.
Ninawasihi sana vijana wenzangu wajifunze mengi kwa kutembelea kumbukumbu za waasisi wa taifa letu kama Nyerere, Karume, Sokoine nk.

Na Gadiola Emanuel, Arusha.

Wilhelm Francis Gidabuday ni kati ya vijana waliotangaza nia ya kugombea ubunge jimbo la Hanang kwa tiketi ya CHADEMA.

B
Mambo makuu atakayosimamia iwapo atapata ridhaa ya chama hatimaye wananchi wa Hanang ni pamoja na;

(1)ARDHI: Hanang kumekuwa na tatizo sugu la uwiano wa upatikanaji wa haki katika baraza zote za ardhi kuanzia kijiji kata hadi wilayani. Pia mgogoro sugu wa mashamba ya Nafco, "nitatafuta haki sawia kwa wakulima na wafugaji, pia nitafuatilia kesi ya msingi iliyofunguliwa dhidi ya Canada katika mahakama ya kimataifa"

C
(2)MAJI: Ufisadi wa watendaji wa serikali kwa kula njama na bodi za maji zimesababisha shida ya maji sehemu kubwa ya Hanang. "Huu ni mfano ambao mimi mwenyewe nimewahi kupambana nayo, nitasafiri popote duniani kupata ufadhili wa kuweka miundo mbinu ya kudumu Hanang iondokane na aibu hii iliyosababishwa na uongozi wa kifisadi wa CCM"

D
(3)AFYA: Hanang kuna hospitali moja tu ya wilaya ambayo haina dawa, vitanda hata neti za kuzuia mbu! Mbunge wa Hanang akiugua anaenda India, wanahanang tuende wapi? "Nitahakikisha ruzuku zote zinazotolewa kwa ajili ya mfuko wa afya inatumika ipasavyo sambamba na kujenga vituo vya afya (dispensaries) ngazi ya kata kama ambavyo sekondari zimejengwa kata zote bila kusahau kusomesha manesi na madaktari wapya"

(4)ELIMU: Maendeleo ya binadamu hutegemea elimu, matokeo ya wanafunzi wa Hanang hayakuwa mazuri kwa miaka ya karibuni. "Kwa kushirikiana na wataalam na wadau wa elimu kuboresha taasisi zilizopo kwa kuongeza maabara ili elimu ya vitendo iongezee kasi nadharia, pia kusaka namna mbadala wa kuwaongezea motisha wakufunzi"

(5)MAZINGIRA: Msitu wa Hanang na mabonde yake, Ziwa Bassotu, Ziwa la Chumvi Gendabi na Balangdalalu ni utajiri usiopimika aliyotupa mwenyezi Mungu. "Nitahakikisha sheria zilizotungwa na bunge zinazolinda mazingira zinafuatwa ipasavyo bila kuathiri huduma kwa wananchi"

(6)MICHEZO: Hanang ni wilaya iliyofanya vizuri katika riadha miaka ya nyuma, "mimi ni mtaalam wa Elimu ya Viungo yaani Physical Education, nimehusika sana katika kuandaa michanganuo ya Chama cha Riadha Tanzania japo sihusiki katika maamuzi, mimi nitahakikisha sheria ya BMT (act # 12/1967) inafanyiwa marekebisho ili tuboreshe michezo kuanzia mashuleni ili tuletee sifa taifa letu katika mashindano ya kimataifa".

Michezo ni ajira, ni afya, ni elimu, ni ukakamavu, ni uzalendo, ni utaifa nk.

HISTORIA KWA UFUPI:

JINA KAMILI;                Wilhelm Francis Gidabuday

NYUMBANI;
Nangwa na Arusha, alioa tangu 1995.

Mawasiliano;
S.L.P  81, Nangwa, HanaSimu 0786778421

KAZI;                   Mkufunzi mchepuo wa michezo (Physical Education Instructor)

ELIMU;                  Msingi - Nangwa (1980-1986)                   Sekondari - Balang'da Lalu (1988-1991)
                                        ELIMU YA JUU;            -Riverside Community College, California
-Life University, Atlanta, GA. (1995/97)

MICHEZO;        
-1993 na 1994 bingwa wa mbio za nyika na za uwanja California
                                      --Bingwa wa mashindano kadhaa duniani ikiwemo Los Angeles Super Bowl 10k Marekani
                                      KAZI;
-Gardena Reebok California -1995 hadi 1999
                                        -New Balance -1999 hadi 2002 California
                                        -Brooks Inc - 2003 hadi 2005 California

KAZI HADI SASA;
-Mratibu wa Sokoine Marathon
-Muandaaji wa program za kimichezo chini ya Riadha Tanzania (RT)

G+1
Wilhelm Gidabuday akiwa na Wazazi wake na Marafiki Zake huko Hanang

Wilhelm Francis Gidabuday ni kati ya vijana waliotangaza nia ya kugombea ubunge jimbo la Hanang kwa tiketi ya CHADEMA.
Mambo makuu atakayosimamia iwapo atapata ridhaa ya chama hatimaye wananchi wa Hanang ni pamoja na;

(1)ARDHI: Hanang kumekuwa na tatizo sugu la uwiano wa upatikanaji wa haki katika baraza zote za ardhi kuanzia kijiji kata hadi wilayani. Pia mgogoro sugu wa mashamba ya Nafco, "nitatafuta haki sawia kwa wakulima na wafugaji, pia nitafuatilia kesi ya msingi iliyofunguliwa dhidi ya Canada katika mahakama ya kimataifa"

G+2
Mr & Mrs Wilhelm Gidabuday wakiwa na Tabasamu la Uhakika

(2)MAJI: Ufisadi wa watendaji wa serikali kwa kula njama na bodi za maji zimesababisha shida ya maji sehemu kubwa ya Hanang. "Huu ni mfano ambao mimi mwenyewe nimewahi kupambana nayo, nitasafiri popote duniani kupata ufadhili wa kuweka miundo mbinu ya kudumu Hanang iondokane na aibu hii iliyosababishwa na uongozi wa kifisadi wa CCM"

(3)AFYA: Hanang kuna hospitali moja tu ya wilaya ambayo haina dawa, vitanda hata neti za kuzuia mbu! Mbunge wa Hanang akiugua anaenda India, wanahanang tuende wapi? "Nitahakikisha ruzuku zote zinazotolewa kwa ajili ya mfuko wa afya inatumika ipasavyo sambamba na kujenga vituo vya afya (dispensaries) ngazi ya kata kama ambavyo sekondari zimejengwa kata zote bila kusahau kusomesha manesi na madaktari wapya"

(4)ELIMU: Maendeleo ya binadamu hutegemea elimu, matokeo ya wanafunzi wa Hanang hayakuwa mazuri kwa miaka ya karibuni. "Kwa kushirikiana na wataalam na wadau wa elimu kuboresha taasisi zilizopo kwa kuongeza maabara ili elimu ya vitendo iongezee kasi nadharia, pia kusaka namna mbadala wa kuwaongezea motisha wakufunzi"

(5)MAZINGIRA: Msitu wa Hanang na mabonde yake, Ziwa Bassotu, Ziwa la Chumvi Gendabi na Balangdalalu ni utajiri usiopimika aliyotupa mwenyezi Mungu. "Nitahakikisha sheria zilizotungwa na bunge zinazolinda mazingira zinafuatwa ipasavyo bila kuathiri huduma kwa wananchi"

(6)MICHEZO: Hanang ni wilaya iliyofanya vizuri katika riadha miaka ya nyuma, "mimi ni mtaalam wa Elimu ya Viungo yaani Physical Education, nimehusika sana katika kuandaa michanganuo ya Chama cha Riadha Tanzania japo sihusiki katika maamuzi, mimi nitahakikisha sheria ya BMT (act # 12/1967) inafanyiwa marekebisho ili tuboreshe michezo kuanzia mashuleni ili tuletee sifa taifa letu katika mashindano ya kimataifa".
Michezo ni ajira, ni afya, ni elimu, ni ukakamavu, ni uzalendo, ni utaifa nk.

No comments:

Post a Comment

Tuwasiliane

Name

Email *

Message *

Contact Form

Name

Email *

Message *