Matukio : Mhe. Joshua Nassari Amenusurika kifo kwa Ajali ya Helkopta Jimboni Kwake - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

Wednesday, 8 July 2015

Matukio : Mhe. Joshua Nassari Amenusurika kifo kwa Ajali ya Helkopta Jimboni Kwake


Habari zilizotufikia na kuthibitishwa na Katibu wa Mbunge wa Arumeru Mashariki zinaeleza kuwa Mbunge Joshua Nassari pamoja na abiria wengine wawili na rubani wao wamenusurika kifo baada ya helkopta waliyokuwa wakisafiria kuhamasisha uandikishaji Jimboni kuanguka jioni ya 7/7 /2015.
Taarifa zinaeleza kuwa helkopta hiyo imeanguka katika kijiji cha Leguruki Wilayani Arumeru Mashariki baada ya hali ya hewa kuwa mbaya.
Nassari na majeruhi wengine wamewahishwa hospitali ya Selian Jijini Arusha kwa matibabu ya majeraha kiasi waliyoyapata.
Blog hii inaendelea kufuatilia tukio hili kwa karibu na kukujuza kila kitu.

No comments:

Post a Comment