
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akitoa sadaka kwa
Watoto Yatima wa kiumewa Kituo cha Kulelea Watoto Yatima cha Rahman
kiliopo Chang’ombe Mjini Dodoma hapo kwenye makazi yake Mtaa wa Farahani
Mjini Dodoma.Kulia ya Balozi Seif Ali Iddi ni Mkewe Mama Asha Suleiman
Iddi.

Balozi
Seif Ali Iddi akitoa sadaka kwa Watoto Yatima wa Kike wa Kituo cha
Kulelea Watoto Yatima cha Rahman kiliopo Chang’ombe Mjini Dodoma baada
ya kufutari nao pamoja.

Baadhi
ya Watoto Yatima wa Kituo cha Kulelea Watoto Yatima cha Rahman kiliopo
Chang’ombe Mjini Dodoma wakipata futari ya pamoja iliyoandaliwa na
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif katika Makaazi yake
yaliyopo Mtaa wa Farahani Mjini Dodoma. Picha na – OMR – ZNZ.
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amesisitiza umuhimu wa
Waumini wa Dini ya Kiislamu kuendelea kujenga utamaduni wa kufutari
pamoja ili kudumisha utaratibu uliotiliwa nguvu na Kiongozi wa Dini hiyo
Mtume Muhammad { SAW } na kuendelezwa na maswahaba waliomfuata.
Balozi
Seif ametoa sisitizo hilo kwenye hafla ya Futari ya pamoja
aliyowaandalia Watoto Yatima wanaolelewa katika Kituo cha malezi ya
Watoto yatima cha Kiislamu cha Rahman Kiliopo Chang’ombe Mjini Dodoma.
Futari hiyo ambayo pia ilihudhuriwa na baadhi ya viongozi wa Dini ya
Kiislamu wa Mji wa Dodoma wakiambatana na baadhi ya Viongozi wa Serikali
na Kisiasa ilifanyika katika Makazi yake yaliyopo Mtaa wa Farahani
Mjini Dodoma.
Balozi
Seif alisema mijumuiko hiyo ya waislamu mara kadhaa husaidia kuongeza
upendo, ushirikiano na mahaba baina yao jambo ambalo huongeza nguvu za
pamoja katika jitihada zao za kusimamisha Dini ya Mwenyezi Muungu.
Akiwapatia
sadaka katika kujiandaa kusherehekea siku kuu ya Iddi El - Fitri
wanafunzi hao wa Chuo cha Malezi ya Kiislamu ya watoto Yatima cha Rahman
Balozi Seif aliwaombea kusherehekea siku kuu hiyo kwa amani,salama na
upendo.
Akitoa
shukrani kwa niaba ya waalikwa wa futari hiyo Sheikh Shaaban Kitila wa
Masjid Nunge alimpongeza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif
kwa ukarimu wake wa kuwakusanya wauminbi wenzake kwenye futari ya
pamoja.
Balozi
Seif amejiwekea utaratibu wa kufutari pamoja na Watoto hao wa Kituo cha
kulelea Watoto yatima Mjini Dodoma napokuwa katika shughuli zake za
kikazi akiwa Mjini Humo ndani ya Mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Wakati
Kumi la Pili ya Maghfira likimalizika na kuingia kumi la Mwisho la
Kuachwa huru na Moto ndani ya Mfungo wa mwezi Mtukufu wa Radhani waumini
wa Dini ya Kiislamu wamekuwa wakiendelea kujumuika katika futari ya
pamoja katika maeneo mbali mbali hapa Nchini.
Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
8/7/2015.
No comments:
Post a Comment