Afisa
Mahusiano na Masoko wa Fastjet, Lucy Mbogoro (kulia) akifafanua jambo
kwa wandishi wa habari (Hawapo pichani) wakati wa mkutano wa wandishi wa
habari akielezea kampuni hiyo ilivyoweza kusaidia sanaa kwa Tanzania na
Afrika. Kushoto kwake ni CEO wa ZIFF, Prof. Martin Mhando.
Na Andrew Chale.
Shirika
la ndege la Fastjet limeendelea kupanua wigo wake kwa kuanzisha ‘rout’
zaidi za safari zake ikiwa ni kuunganisha Afrika kuwa moja.
Kwa
mujibu wa Afisa Mahusiano na Masoko wa Fastjet, Lucy Mbogoro anasema
kampuni hiyo inatarajia kuizindua rasmi safari zake kwa kwenda, Malawi.
“Julai
27, Fastjet tutazindua rasmi safari ya kutoka Dar es Salaam-Lilongwe
Malawi. Hii inakuwa ni ‘rout’ yetu ya tano katika safari zetu za
Kimataifa ndani ya Afrika lengo ni kufikia nchi mbalimbali za Afrika.”
Anabainisha Lucy Mbogolo.
Hata
hivyo anabainisha kuwa, wanaendelea kutoa elimu mbalimbali kwa wateja
wao juu ya huduma ya Fastjet Ambayo imeendelea kuwa bora zaidi kila
kukicha huku akisisitiza kwa wateja kufanya ‘booking’ mapema pamoja na
kuzielewa sheria na taratibu za usafirishaji wa anga.
Awali
Fastjet ilianzia na safari za ndani za kusafirisha abiria ‘rout’ za
Mwanza – Dar, Kilimanjaro – Dar na Mbeya – Dar sasa hivi wamevuka mipaka
zaidi kwa nchi za Afrika zikiwemo, kati ya Dar – Johannesburg, Dar –
Lusaka, Dar – Harare,Dar – Entebbe nah ii inayotarajiwa kuzinduliwa wiki
ijayo ya Dar-Lilongwe.
Aidha,
Lucy Mbogoro alibainisha kuwa Fastjet itaendelea kusaidia kukuza sekta
ya sanaa nchini na Bara la Afrika kwa kuwaunganisha wadau wa sekta hiyo
ikiwemo wasanii wa filamu, muziki na sanaa kwa ujumla.
Lucy
Mbogoro anasema hayo ambaapo kwa mwaka huu ni mwaka wa pili mfululizo
wakiendelea kudhamini tamasha la Filamu za nchi za majahazi maalufu kama
ZIFF. Mwanamuziki
wa Kimataifa, Moussa Diallo kutoka Mali (kushoto), akifafanua jambo kwa
wandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa mkutano wa wandishi wa
habari. Kulia kwake ni Afisa Mahusiano na Masoko wa Fastjet, Lucy
Mbogoro ambao wamedhamini tamasha hilo kwa mwaka wa pili mfululizo kwa
upande wa usafirishaji.. Afisa
Mahusiano na Masoko wa Fastjet, Lucy Mbogoro akizungumza na waandishi
wa habarimuda mfupi baada ya kumalizika kwa mkutano huo.. (Picha zote na
Andrew Chale.)moja ya ndege za Fastjet kama inavyoonekana pichani.
No comments:
Post a Comment